Jumanne, 31 Desemba 2024

TANGA, KITUO CHA UTALII WA KIHISTORIA NA KIUTAMADUNI CHENYE MCHANGO MKUBWA KWA UCHUMI NCHINI TANZANIA.

Mkoa wa Tanga ni eneo lenye historia na utajiri wa kitamaduni, likiwa na vivutio vya kipekee vinavyovutia watalii wa ndani na nje ya nchi. Baadhi ya vivutio maarufu vya utalii mkoani Tanga ni Mapango ya Amboni, ambayo ni mapango makubwa zaidi Afrika Mashariki, na mji wa kihistoria wa Pangani wenye urithi wa kihistoria wa biashara ya utumwa na harakati za uhuru. 

 

Pia, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ni kivutio adimu kinachochanganya mandhari ya wanyamapori na fukwe za bahari, huku Visiwa vya Maziwe vikivutia kwa shughuli za kuogelea, kupiga mbizi, na uchunguzi wa viumbe wa baharini. Aidha, Urithi wa Mji Mkongwe wa Tanga unabeba thamani ya kihistoria inayovutia watafiti na wageni.  

 

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023, Tanga ilipokea jumla ya watalii 150,000, ambapo 30% walikuwa wageni kutoka mataifa mbalimbali. Sekta ya utalii ilichangia takriban TZS bilioni 25 katika uchumi wa mkoa, huku ikitoa ajira zaidi ya 10,000 kwa wakazi wa eneo hilo moja kwa moja.  

 

Vivutio hivi vinaendelea kushikilia nafasi muhimu katika kukuza utalii endelevu, huku serikali na wadau wakihamasisha uwekezaji zaidi ili kuboresha miundombinu na huduma za utalii mkoani Tanga. 

Ijumaa, 27 Desemba 2024

UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, TAKWIMU NA MAFANIKIO YA MIAKA MITATU (2021-2023)

Tanzania imekuwa ikishuhudia ukuaji thabiti wa uchumi kwa miaka kadhaa. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ukuaji wa uchumi wa Tanzania ulikuwa kama ifuatavyo:  

 

2021, Uchumi ulikua kwa asilimia 4.9, licha ya changamoto za janga la COVID-19. 

 

2022, Ukuaji uliongezeka hadi asilimia 5.3, ukichochewa na miradi mikubwa ya maendeleo kama SGR, Mwalimu Nyerere Hydropower, na EACOP.  


2023, Uchumi ulionyesha kasi zaidi kwa ukuaji wa asilimia 5.8, ukihamasishwa na ongezeko la uwekezaji wa ndani na nje.  

 

Sekta zilizoongoza katika ukuaji wa uchumi ni pamoja na.. 

Kilimo: Huchangia takriban asilimia 26.9  ya Pato la Taifa (GDP).  

 

Ujenz: Ulichangia kwa asilimia 14.3 kutokana na miradi mikubwa ya miundombinu. 

 

Utalii: Mapato ya utalii yalifikia Dola za Marekani 2.6 bilioni mwaka 2023, yakirejea kutoka athari za COVID-19.  

 

Ukuaji huu umeimarisha maisha ya Watanzania, kupunguza umaskini, na kuimarisha huduma za msingi kama elimu, afya, na maji safi.

JE, WAJUA! UMOJA WA WATANZANIA NI MFANO WA KUIGWA NA SIO NDOTO TENA?

Tanzania imeendelea kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kwa kusimamia misingi ya umoja, mshikamano, na utawala wa sheria. Umoja wa kitaifa umebaki kuwa nguzo muhimu katika kuimarisha amani, utulivu, na maendeleo ya nchi, huku ukijengwa juu ya msingi madhubuti wa katiba na sheria za nchi.  

Sheria za Tanzania zimetungwa kwa kuzingatia misingi ya usawa, haki, na kuheshimu utu wa binadamu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imeweka bayana kwamba nchi hii ni moja, yenye watu wa makabila, dini, na tamaduni mbalimbali. Hii imekuwa dira ya kuimarisha mshikamano kwa kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anahisi kuwa sehemu ya taifa bila kujali tofauti zao za kijamii au kiitikadi.  

 

Sheria zinazozuia ubaguzi wa aina yoyote zimeimarisha umoja wa kitaifa. Mathalani, Sheria ya Makosa ya Jinai (Penal Code) inahakikisha kwamba vitendo vyote vya uchochezi wa kikabila, kidini, au kijamii vinakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Hali hii imewezesha Tanzania kudumu katika hali ya amani na utulivu kwa zaidi ya nusu karne tangu uhuru.  

 

Taratibu za kitanzania, kama vile kuheshimu mamlaka za kijamii, kushiriki katika maadhimisho ya kitaifa, na kuzingatia mila na desturi za Watanzania, zimekuwa sehemu muhimu ya kudumisha mshikamano. Maadhimisho kama Siku ya Uhuru, Muungano, na Mashujaa huwakutanisha Watanzania kutoka pande zote za nchi kusherehekea na kuthamini historia ya pamoja.  

 

Aidha, Tanzania imejikita katika sera zinazolenga kuimarisha umoja, kama vile Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inayosisitiza matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia, ambayo imeendelea kuwa kiunganishi kikuu kwa Watanzania wote.  

Umoja huu ni matokeo ya juhudi za pamoja za wananchi na viongozi waliochaguliwa kwa misingi ya demokrasia.  

 

Kwa sasa, Tanzania inajivunia kuwa na mazingira salama ya kibiashara, maendeleo ya miundombinu, na huduma za kijamii ambazo zinawanufaisha watu wa makundi yote. Mfano hai ni utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa, kama vile reli ya kisasa (SGR), mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, na miradi ya maji inayohakikisha Watanzania wanapata huduma muhimu bila ubaguzi.  

 

Ili kuhakikisha kwamba umoja wa Tanzania unadumu kwa vizazi vijavyo, ni muhimu kuendelea kutoa elimu ya uraia, kusimamia haki za binadamu, na kuhakikisha kila mtu anashiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi. Viongozi wa kisiasa, kijamii, na kidini wanapaswa kuendelea kuwa mfano bora wa mshikamano, huku wakiwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuheshimu sheria na taratibu za nchi.  

 

Kwa hakika, umoja wa Tanzania sio ndoto tena, bali ni ukweli unaoishi ndani ya mioyo ya Watanzania. Kwa kushikamana na misingi ya sheria na taratibu, taifa hili linaendelea kuwa kisiwa cha amani na mshikamano katika bara la Afrika.  

 

#SioNdotoTena  

Jumanne, 24 Desemba 2024

JE, MRADI WA MABASI YA MWENDO KASI (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM NI SULUHISHO LA KUDUMU KWA CHANGAMOTO ZA USAFIRI?

Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT) jijini Dar es Salaam ni mojawapo ya miradi muhimu zaidi ya miundombinu nchini Tanzania, ukilenga kuboresha usafiri wa umma na kupunguza changamoto za msongamano wa magari. Tangu kuanzishwa kwake, mradi huu umeleta mabadiliko makubwa kwa wakazi wa jiji hilo.

Awamu ya kwanza ya BRT ilianza kazi rasmi mwaka 2016, ikiwa na kilomita 21.1 za barabara maalum za mwendo kasi, vituo 27 vya kisasa vya mabasi, na daraja kubwa la Tazara. Awamu hii ilihudumia takribani abiria 200,000 kila siku, ikisaidia kupunguza muda wa safari na gharama za usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam. 

 

Utekelezaji wa awamu nyingine za mradi unaendelea kwa kasi. Awamu ya pili, yenye kilomita 20.3 kutoka Mbagala hadi katikati ya jiji, imekamilika kwa asilimia 95, huku gharama za mradi huu zikifikia zaidi ya shilingi bilioni 290. Mabasi yameanza majaribio, na matarajio ni kuanza huduma rasmi hivi karibuni. Awamu hii inatarajiwa kuhudumia wakazi wa maeneo ya kusini mwa jiji, ambayo awali yalikuwa na changamoto kubwa ya usafiri.

 

Awamu ya tatu ya mradi, inayohusisha kilomita 23.6 kutoka Gongo la Mboto hadi Kariakoo kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), imekamilika kwa asilimia 70. Barabara hii itaunganisha maeneo muhimu ya biashara na uchumi, na pia kuboresha usafirishaji wa abiria na mizigo ndani ya jiji.

 

Kwa ujumla, mpango wa BRT unalenga kujenga zaidi ya kilomita 130 za barabara maalum za mwendo kasi. Hadi sasa, zaidi ya kilomita 64 zimekamilika na ziko katika matumizi. Mradi huu unatarajiwa kupunguza muda wa safari kwa wastani wa asilimia 50, kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kutumia mabasi yanayotumia nishati safi, na kuboresha hali ya hewa ya jiji. Pia, unatoa ajira kwa maelfu ya vijana, ikiwa ni pamoja na madereva, wahudumu wa vituo, na mafundi wa matengenezo ya miundombinu.

 

Faida za mradi huu kwa Watanzania ni nyingi. Kwanza, umeongeza ufanisi wa usafiri wa umma kwa kuwapa wananchi chaguo la usafiri wa haraka na salama. Pili, mradi huu umechangia katika kukuza uchumi wa maeneo ya jirani, kwani watu wengi sasa wanaweza kufikia maeneo ya kazi na biashara kwa urahisi. Tatu, umeimarisha hadhi ya Dar es Salaam kama jiji linaloendelea kwa kasi barani Afrika.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, akizungumza hivi karibuni, alisema: "Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ni zaidi ya mradi wa miundombinu. Ni mabadiliko ya kimkakati yanayolenga kuboresha maisha ya kila Mtanzania."

 

Kwa wakazi wa Dar es Salaam, mradi wa BRT ni kielelezo cha maendeleo na matumaini. Kadri awamu mpya za mradi zinapokamilika, BRT itaendelea kuwa nguzo muhimu ya usafiri wa umma nchini Tanzania na mfano wa mafanikio ya kisasa katika sekta ya miundombinu.

 

Alhamisi, 12 Desemba 2024

OFISI YA MKUU WA WILAYA NJENDENGWA, DODOMA: ALAMA YA MAENDELEO CHINI YA UONGOZI WA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Dodoma, Tanzania - Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyopo Njendengwa, ndani ya Jiji la Dodoma, ni mojawapo ya miradi muhimu ya ujenzi iliyotekelezwa katika awamu ya sita ya uongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Jengo hili limejengwa kwa kuzingatia viwango vya kisasa, likiwa na miundombinu ya kisasa inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za utawala na maendeleo kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kukamilika kwa jengo hili ni sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha miundombinu ya kisiasa na kiutawala inaimarishwa, ikiwa ni ishara ya dhamira ya Rais Samia katika kuleta maendeleo yenye tija kwa Taifa.  

Aidha, ujenzi wa ofisi hii ni sehemu ya mpango mpana wa serikali ya awamu ya sita wa kuboresha huduma kwa wananchi kwa kuhakikisha watendaji wa serikali wanakuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi, hatua inayochangia ufanisi wa utoaji huduma na maendeleo katika ngazi za wilaya na mikoa.  

Wananchi wa Dodoma wamesifu juhudi za serikali kwa kuona kuwa Wilaya ya Dodoma imepewa kipaumbele, huku wakibainisha kuwa jengo hili litachochea maendeleo ya kiutawala na kijamii katika eneo hilo.  

KIWANDA CHA KUTENGENEZA NDEGE MOROGORO: MAENDELEO MAKUBWA YA AIRPLANE AFRICA LIMITED

 

Kampuni ya Airplane Africa Limited (AAL), inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech, ilianzisha kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza ndege mwaka 2021 katika eneo la Mazimbu, mkoani Morogoro. Kiwanda hiki ni cha kwanza barani Afrika katika sekta hii. 

Hadi kufikia Desemba 2024, AAL imefanikiwa kuunganisha na kutengeneza zaidi ya ndege tatu aina ya Skyleader 600, zenye uwezo wa kubeba abiria wawili hadi wanne. Ndege hizi zimeanza safari rasmi ndani na nje ya nchi, baada ya kupata cheti cha kuipasisha kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) mnamo Septemba 2024. 


Kiwanda hiki kimeajiri mafundi wengi ambao ni wahitimu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), hivyo kuchangia katika kutoa uzoefu kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu, vyuo vya kati, na vyuo vya ufundi. 

 

Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Uchukuzi, imeonyesha nia ya kusaidia sekta ya anga kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ili kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kama AAL. Hatua hii inalenga kuimarisha uwekezaji na kukuza teknolojia ya utengenezaji wa ndege nchini. 

 

Kwa sasa, ndege zinazotengenezwa na AAL zinaweza kuuzwa katika nchi mbalimbali, na mipango ya baadaye ni kuunda ndege zenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya wawili. 

 

Kwa maelezo zaidi kuhusu kiwanda hiki na shughuli zake, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya Airplane Africa Limited. 

 

 

KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA, WATENDAJI WA MIKOA NA HALMASHAURI ZA MKOA WA MARA WAPIGWA MSASA JUU YA UTAWALA BORA NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA


Wizara ya Katiba na  sheria imeanza kutoa  mafunzo ya utawala Bora  na Uraia kwa kamati za Usalama za Mikoa na Wilaya,wakuu wa idara mbalimbali za Halmashauri na watendaji wa Kata wilayani Rorya Mkoani Mara ili kuwakumbusha kuzingatia Mipaka katika utumishi wa umma na Misingi ya Utawala bora.

 


Akizungumza Wakati wa mafunzo hayo Wilayani Rorya Mkoani mara  Joyce mushi wakili wa serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia nimratibu wa mafunzo wa Elimu ya utawala Bora ambapo amesema Mafunzo hayo nimwendelezo wa mafunzo ambapo yalianzia Mkoa wa Rukwa huku walengwa wakuu wakiwa nikamati za Usalama watendaji wa kata na watumishi wa idara mbalimbali za Halmashauri.

 

Joyce alisema lengo la Mafunzo hayo nikuwakumbusha na kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kuwa na Uelewa wakutekeleza majukumu Yao kwa kufata misingi ya utawala bora na haki za binadamu na demokrasia.

 


"Mafunzo hayo kutolewa niutekelezaji wa Falsafa ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan ya 4R- ya Ujenzi upya(Rebuilding) ambapo tunaamini tukimaliza Mafunzo haya washiriki wote watakuwa wamejengwa upya na Kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha kwa Wananchi"Joyce mushi wakili wa serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria"

 

Robhi Richard wambura Afisa mtendaji kata ya Roche nimiongoni mwa wanaufaika wa mafunzo hayo ambapo amemshukuru Rais DKT Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Katiba na Sheria alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwa chachu ya mabadiliko katika vituo vya kazi kutokana na kipindi cha Nyuma wengi wao walikuwa wanafanya kazi bila kuzingatia miiko na Mipaka yao yakazi.

 


Elimu ya Utawala bora na uraia kwa viongozi wa mamlaka za Serikali za mitaaa inaendelea katika Mkoa wa mara huku ikitarajiwa kufanyika katika Halmashauri zote za Mkoa huo wa Mara 

🇹🇿 MTUMBA YAANDIKA HISTORIA! VIONGOZI NA WANANCHI WASHUHUDIA HATUA MPYA YA MAENDELEO DODOMA

  DODOMA | OKTOBA 30, 2026 Ni tukio la kihistoria katika safari ya maendeleo ya Tanzania! Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wamekusanyi...