Jumapili, 1 Juni 2025

UMUHIMU WA ZIARA YA RAIS WA TFF KUKAGUA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU ARUSHA – KWA ULIMWENGU WA SOKA NA USTAWI WA TAIFA

Ziara ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu katika kata ya Olmoti, Arusha, ni tukio la msingi lenye uzito mkubwa katika nyanja mbalimbali – michezo, uchumi, utalii na hadhi ya taifa kimataifa. 

1. Maandalizi ya AFCON 2027: Taifa la Tanzania Katika Ramani ya Soka Afrika

Uwanja huu unajengwa mahsusi kwa ajili ya mashindano ya AFCON 2027, ambayo Tanzania ni mwenyeji mwenza. Ujenzi huu na ukaguzi wa viongozi wakuu unahakikisha:

  • Taifa linatimiza masharti ya CAF kuhusu miundombinu bora ya michezo.

  • Tanzania inaonesha umoja wa kitaifa na utayari wa kitaifa kupokea mataifa mengine.

  • Tunajenga historia kwa kuwa wenyeji wa tukio kubwa zaidi la soka barani Afrika.


2. Kukuza Michezo, Kuibua Vipaji na Kuendeleza Vijana

Kwa kuwa uwanja huu utabaki kama urithi wa kimichezo:

  • Utawasaidia vijana wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kufanya mazoezi na kucheza katika mazingira ya kiwango cha juu.

  • Klabu na shule zitakuwa na fursa ya kutumia uwanja bora, hivyo kuongeza ushindani na ubora wa wachezaji wa ndani.

  • Vipaji vitakuza soko la ndani na la kimataifa kwa wachezaji wetu.

     

3. Kuleta Ustawi wa Kiuchumi wa Mkoa wa Arusha na Taifa kwa Ujumla
  • Ajira: Ujenzi huu unatoa ajira za muda kwa mafundi, vijana, na wasambazaji wa vifaa.

  • Utalii wa Michezo: Uwanja huu utavutia wageni wa ndani na nje, kuongeza mapato ya hoteli, usafiri, biashara ndogo, na huduma za utalii.

  • Mzunguko wa pesa: Maandalizi ya AFCON yatachochea biashara mbalimbali – kuanzia vinywaji hadi mavazi ya michezo.

 


4. Kuimarisha Hadhi ya Tanzania Kimataifa

  • Kupitia AFCON 2027 na maendeleo ya viwanja kama huu wa Olmoti, Tanzania inaongeza uwezo wa kupokea matukio ya kimataifa.

  • Taifa linaonesha kwamba linaweza kuwekeza katika miundombinu ya kisasa, ambalo ni hitaji la msingi kwa maendeleo ya kisasa.

 5. Ushirikiano wa Serikali na Mashirikisho ya Michezo

Ziara ya Wallace Karia akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Methusela Ntonda, inaashiria:

  • Umoja baina ya sekta ya umma na michezo katika kufanikisha ajenda ya kitaifa.

  • Ushirikiano huu unaongeza uwajibikaji, ufuatiliaji, na ubora wa utekelezaji wa miradi ya kitaifa ya michezo.

 


6. Ujenzi wa Taifa Lenye Afya na Maadili Kupitia Michezo

Michezo huchangia kuhamasisha:

  • Maadili ya nidhamu, uzalendo, na mshikamano, hasa miongoni mwa vijana.

  • Afya ya jamii, kupunguza matumizi ya mihadarati, na kupunguza makosa ya jinai kwa vijana kupitia shughuli za kujenga.

Ziara ya Rais wa TFF kukagua uwanja wa Olmoti ni zaidi ya ukaguzi wa kisoka. Ni ishara ya mwelekeo mpya wa Tanzania, nchi inayotumia michezo kama nguzo ya maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kidiplomasia. Huu ni uwekezaji wa kizazi, si tu kwa ajili ya mechi za AFCON, bali kwa ajili ya taifa imara, lenye afya na mshikamano wa kudumu.



"Tanzania si tu inajenga uwanja, bali inajenga hadhi, fursa na mustakabali wa vijana wake kupitia mpira wa miguu."


Jumanne, 27 Mei 2025

JE, UNAJUA TANZANIA IMEJENGA ZAIDI YA KM NGAPI ZA BARABARA MPAKA SASA?

 






TANZANIA YETU, FAHARI YETU: KAZI, UTU NA UPENDO NDIYO UTAMBULISHO WETU.

 












MWENGE WA UHURU WAZINDUA NEEMA YA MAJI TANDAHIMBA – VIJIJI 5 KUFAIDIKA

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tandahimba umetenga Shilingi 452,500,000 kwa ajili ya kuchimba visima vitano vya maji safi na salama katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma, Mchangani na Michenjele, kwa lengo la kuondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo hayo.


Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba, Falaura Kikusa alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya Programu Maalumu ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inayolenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama.

“Mradi huu ni mkakati maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kupunguza adha ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hii muhimu. Utekelezaji wake ulianza Mei 2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 2025 kutokana na changamoto mbalimbali, licha ya mpango wa awali kumalizika Disemba 2024,” alisema Kikusa.

Kikusa alieleza kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 76, ambapo miundombinu ya maji ikiwemo usimikaji wa matanki ya lita 10,000 imekamilika katika vijiji viwili vya Mivanga na Lyenje, huku usimikaji wa pampu na mifumo ya nishati ya jua ukiwa umefanyika katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma na Mchangani.


Kwa mujibu wa Kikusa, gharama ya kisima kimoja ni Shilingi 90,500,000 na hadi sasa Shilingi 124,106,686.40 kati ya fedha zilizotengwa tayari zimelipwa. Fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo mpango wa Lipa kwa Matokeo, Mfuko wa Taifa wa Maji na michango ya wadau wa maendeleo.


Aidha, alisema mradi huo umetoa ajira za muda mfupi kwa wananchi wa maeneo husika wakiwemo mafundi, wapishi, na madereva, huku pia ukichochea maendeleo ya kilimo na kusaidia kupunguza magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara.


Katika kijiji cha Mivanga, kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha maji lita 372,000 kwa siku. Wananchi wa vijiji hivyo wametoa maeneo ya ujenzi wa visima hivyo bila fidia, yenye thamani ya takriban Shilingi 2,500,000.


Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed ameishukuru serikali kupitia RUWASA kwa kutekeleza mradi huo muhimu na kusisitiza kuwa umeleta afueni kubwa kwa wananchi waliokuwa wanatumia gharama kubwa na muda mwingi kutafuta maji.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujali ustawi wa wananchi wa Tandahimba na kuwataka wakazi wa vijiji walionufaika na mradi huo kushirikiana na serikali kuutunza ili udumu kwa muda mrefu.


Mkazi wa kijiji cha Mivanga, Bi. Asha Seleman alisema mradi huo umesaidia kupunguza gharama za maisha kwa wakazi wa kijiji hicho kwani hapo awali walikuwa wananunua ndoo moja ya maji ya lita 20 kwa Shilingi 1,000.

MUHAS KUANZA MAFUNZO MAALUM KWA GYM INSTRUCTORS ILI KUBORESHA USALAMA WA MAZOEZI KWA WAGONJWA

 

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kuanza kutoa mafunzo maalum ya kitaalamu kwa wakufunzi wa mazoezi ya viungo (gym instructors) na wasimamizi wa kumbi za mazoezi (fitness managers),ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wateja wanaopelekwa kufanya mazoezi kwa sababu za kitabibu.


Akizungumza leo Mei21,2025 wakati wa uzinduzi wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa afya ya moyo bila malipo katika Kampasi ya MUHAS Mloganzila,Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa moja amesema mpango huo unalenga kulinganisha huduma za mazoezi ya viungo ya viwango vya kitaifa vya afya.


“Uzoefu unaonesha kuwa watu wengi huanza mazoezi bila ushauri wa kitabibu, jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa afya hususani moyo,” amesema Profesa Kamuhabwa.


Ameongeza,“Lengo letu ni kuwajengea uwezo waendeshaji wa kumbi za mazoezi ili waweze kutoa huduma kwa kufuata taratibu za kitaalamu za afya,”


Ameonya suala la jamii kufanya mazoezi bila usimamizi wa kitabibu kunaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha ghafla kwa watu wenye magonjwa ya moyo au matatizo mengine ya kiafya yaliyofichika.


Profesa Kamuhabwa amesema kama sehemu ya mpango huo, MUHAS itazindua kituo kipya cha mazoezi ya viungo mapema wiki hii, ambacho kitakuwa kinatoa vyeti vya mazoezi kama ilivyo kwa dawa zinazotolewa kwa agizo la daktari.


Amesema mafunzo hayo pamoja na uanzishaji wa gym hiyo ni sehemu ya jitihada za kuboresha kiwango cha huduma za mazoezi ya viungo nchini na kupunguza hatari za kiafya kutokana na mazoezi yasiyo na miongozo ya kitaalamu.


Akizungumzia kambi ya uchunguzi inayoendelea, Profesa Kamuhabwa amesema shughuli mbalimbali zinazofanyika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya Kituo cha Umahiri cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni pamoja na huduma za magonjwa ya moyo, kinga na tiba kwa wale watabainika kuwa na matatizo ya moyo.


Kwa upande wake, mtaalamu wa fiziolojia Irine Mngolokolo,amesema gym hiyo mpya imeundwa mahsusi kwa ajili ya watu wenye changamoto za kiafya.


Irene ambaye pia ni msaidizi wa kufundisha katika kituo hicho amesisitiza umuhimu wa kuanza mazoezi kwa mpango maalum uliopangwa na mtaalamu, iwe ni ya aerobic au anaerobic, kulingana na mahitaji ya mhusika.


Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Emmanuel Balandya, amesema kuwa mafunzo ya wataalamu wa afya ya moyo ni moja ya vipaumbele vikuu vya MUHAS.

BAJETI YA UVUVI 2025/26 YASISIMUA, TEKNOLOJIA, MAFUNZO NA MIKOPO KWA WAVUVI

 




NGUVU MPYA KWA WAVUVI NA WAFUGAJI: SERIKALI YAJIBU KWA BAJETI YA KIMKAKATI






 

🇹🇿 MTUMBA YAANDIKA HISTORIA! VIONGOZI NA WANANCHI WASHUHUDIA HATUA MPYA YA MAENDELEO DODOMA

  DODOMA | OKTOBA 30, 2026 Ni tukio la kihistoria katika safari ya maendeleo ya Tanzania! Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wamekusanyi...