RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA MKUTANO MKUU WA 39 WA ALAT JIJINI DODOMA
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Samia amesisitiza umuhimu wa serikali za mitaa katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi. Ameeleza kuwa serikali yake itaendelea kuimarisha ushirikiano na ALAT ili kuhakikisha kuwa changamoto zinazoikumba sekta ya utawala wa mitaa zinapatiwa suluhisho la kudumu.
Aidha, Rais Samia amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwazi, na uwajibikaji ili kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi. Pia amewahimiza kutumia teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi na uwazi katika utawala wa mitaa.
Mkutano huu wa ALAT umehudhuriwa na viongozi wa serikali, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, madiwani, na wadau mbalimbali wa maendeleo. Pamoja na kujadili masuala ya utawala bora katika serikali za mitaa, mkutano huu pia umeweka mkakati wa kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi katika ngazi za halmashauri nchini.
Kwa upande wao, viongozi wa ALAT wamemshukuru Rais Samia kwa uongozi wake thabiti na dhamira yake ya kuimarisha utawala wa mitaa kwa maendeleo endelevu ya nchi.
Mkutano huu wa 39 wa ALAT umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana mawazo, kutathmini mafanikio na changamoto, pamoja na kupanga mikakati ya kuimarisha utawala bora katika serikali za mitaa.
Mkutano huu ukawe wenye tija katika kuboresha ushirikiano baina ya Wananchi na viongozi wa serikali za mitaa katika kuliletea maendeleo
ReplyDelete#SisiNiTanzania
#MatokeoChanya
#Katiba_sheria
#MsLAC
#DrSSH
#Kaziiendelee
Mkutano huu wa 39 wa ALAT imeonekana kuwa na tija kwa Jumuiya ya ALAT lakini pia kwa wananchi ambao waliisikiliza HOTUBA ya Mh. Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN iliyojaa maneno ya kujenga Tanzania mpya kimaendeleo huku ikisisitiza uwajibikaji kwa viongozi katika kuwatumikia wananchi na sio kuwa chanzo cha migogoro, kwani serekali za mitaa kupitia halmashauri imekuwa ni muhimili mkubwa katika jamii.
ReplyDelete#SSH #matokeochanya #SISINITANZANIA #mslac #kazinaututunasongambele #katibanasheria #ALAT
Mkutano huu ni chachu ya maendeleo ambao utaimarisha utawala bora wa serikali za mitaa #ssh ##SisiNiTanzania #NaipendaNchiYangu #matokeochanya #katibaNaSheria #kaziiendelee #NchiYanguKwanza
ReplyDeleteSerikali za mitaa ni moyo wa taifa...maana kazi kubwa inafanyika huko na utekelezaji wa bajeti zote za fedha
ReplyDelete