Alhamisi, 13 Februari 2025

TANZANIA KUANDAA MKUTANO WA 73 WA BARAZA LA KIMATAIFA LA VIWANJA VYA NDEGE AFRIKA (ACI-AFRICA)

Arusha, Tanzania – Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (Airports Council International - ACI) kwa Kanda ya Afrika, ambapo maandalizi yanaendelea kwa kasi ili kufanikisha tukio hilo kubwa la kimataifa.  

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kisongo, Jijini Arusha, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema mkutano huo utafanyika kuanzia Aprili 24 hadi 30, 2025, na utahusisha washiriki zaidi ya 400 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika na kwingineko.  

 

“Mkutano huu wa siku saba utaanza na Mkutano Mkuu, ikifuatiwa na Mikutano ya Bodi na Mikutano ya Kamati mbalimbali za kitaalam, pamoja na maonesho ya wadau wa sekta ya usafiri wa anga,” amesema Prof. Mbarawa. 

 

Katika mkutano huo, washiriki watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo Arusha, ambapo siku moja imetengwa kwa ajili ya takriban wageni 300 kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro, huku wengine wakielekea kwenye vituo mbalimbali vya utalii jijini Arusha.  

 

Kaulimbiu ya mkutano huu ni "Katika Kuelekea Wakati Ujao Bora wa Kijani: Kutumia Usafiri wa Anga Endelevu na Utalii kwa Ustawi wa Kiuchumi," ikilenga kuangazia maendeleo endelevu katika sekta ya usafiri wa anga na mchango wake katika utalii na uchumi wa Afrika.  

 

Tanzania, kupitia mkutano huu, inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha sekta ya usafiri wa anga na kulinda mazingira, huku ikijitokeza kama kitovu cha mikutano mikubwa ya kimataifa na biashara barani Afrika.

Maoni 3 :

  1. #ssh #tanzaniayangu #matokeochanya #sisinitanzania #mslac #kaziiendelee

    JibuFuta
  2. Msaada wa Kisheria Kwa haki, Usawa, Amani na maendeleo
    #HayaNdioMatokeoChanya+
    #Katiba_sheria
    #MSLAC
    #DrSSH
    #Kaziiendelee

    JibuFuta
  3. Naipenda nchi yangu #ssh #sisinitanzania #matokeochanya #katibanasheria #nchiuangukwanza #kaziiendelee

    JibuFuta

VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA

Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...