MAFUNZO YA WAJUMBE WA KAMATI YA USALAMA KUHUSU ELIMU YA URAIA NA UTAWALA BORA YANAYORATIBIWA NA WIZARA YA SHERIA NA KATIBA YANAFANYIKA MKOANI IRINGA
Iringa, Desemba 11, 2024
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Herry James, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, amefungua rasmi mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati za Usalama za Mkoa wa Iringa. Mafunzo haya, yanayoratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, yanafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 13 Desemba 2024.
Akizungumza katika hafla hiyo, Herry James aliwashukuru waandaaji na washiriki wa mafunzo haya kwa kujitokeza kwa wingi, akisisitiza umuhimu wa mafunzo haya katika kuongeza uelewa wa masuala ya demokrasia, haki za binadamu, utawala bora, na majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama.
![]() |
Mratibu wa Mafunzo hayo Bi Dorice Dario,Wakili Mkuu daraja la kwanza (principal state Attorney) kutoka idara ya Katiba na ufuatiliaji haki Wizara ya katiba na sheria. |
“Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo viongozi katika ngazi mbalimbali za utawala ili kuhakikisha tunazingatia misingi ya utawala bora, haki za binadamu, na demokrasia kwa vitendo,” alisema.
Kiongozi huyo alibainisha kuwa mafunzo haya yanahusisha wajumbe wa Kamati za Usalama za Mkoa na Wilaya, baadhi ya wataalam wa Halmashauri, na Watendaji wa Kata zote za Mkoa wa Iringa. Pia alieleza kuwa mafunzo ya ngazi ya Halmashauri yatafanyika kwa Kamati za Usalama za Wilaya, wataalam, na watendaji wa kata.
Changamoto Zinazokabili Mkoa wa Iringa
Katika hotuba yake, Herry James alieleza changamoto mbalimbali zinazokabili Mkoa wa Iringa, zikiwemo uelewa mdogo wa haki za binadamu, mila na desturi kandamizi, vitendo vya ukatili wa kijinsia, pamoja na imani za kishirikina. Alitoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kushirikiana kutatua changamoto hizi kwa kushirikisha maarifa watakayopata.
Msaada wa Kisheria wa Mama Samia
Akigusia kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign), alisema kuwa kampeni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika mikoa mbalimbali. Alitoa wito kwa viongozi na watendaji wa Mkoa wa Iringa kushiriki kikamilifu kuhamasisha wananchi kutumia huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure kupitia kampeni hiyo.
Akihitimisha hotuba yake, Herry James aliwahimiza washiriki kuhakikisha kuwa maarifa yatakayotolewa yanakuwa chachu ya mabadiliko katika utendaji wao wa kila siku. “Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa elimu hii inasambazwa kuanzia ngazi ya familia hadi sehemu za kazi ili kujenga jamii yenye haki, amani, na utawala bora,” alisisitiza.
Aliwatakia washiriki mafunzo yenye tija na mafanikio, huku akitoa pongezi kwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na wawezeshaji wote kwa kufanikisha mafunzo haya.
Mafunzo haya sasa yamefunguliwa rasmi na yanatarajiwa kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi wa haki za binadamu, utawala bora, na demokrasia ndani ya Mkoa wa Iringa.
Mungu Ibariki Tanzania!
Hakika malengo ni makubwa kwa mustakabali wa taifa japo vijijini na mijini sheria nyingi hazifahamiki na watu wanaishi kwa mazoea lakini kwa kampeni hii wananchi watafahamu kuhusu mambo mengi sana ya kisheria ili kuweza kukabiliana na changamoto zinapojitokeza #SSH
ReplyDelete#sisi ni Tanzania
Pamoja na uwepo wa changamoto zilizoainishwa na mhe Mkuu wa Wilaya ya Iringa kama vile ukatili ,Unyanyasaji wa kijinsia na Tamaduni na mila kandamizi basi Uwepo wa MAMA SAMIA LAGAL AID CAMPAIGN itakua suluhisho la changamoto hizo zote..#SisiNiTanzania #SSH #MSLAC #KatibaNaSheria
ReplyDeleteWizara ya Katiba na Sheria inafanya kazi Kubwa katika kuhakikisha Elimu ya utawala Bora, demokrasia na haki za binadamu zinatolewa Kwa viongozi wa ngazi zote ili kuimarisha Utoaji wa haki Kwa Wananchi.
ReplyDeleteNijambo jema sana kujenga uzoefu na kuimarisha serikali inayoendeshwa kwa haki na usawa #sisinitanzania #matokeochanya zee
ReplyDeleteLengo kubwa wananchi tupate uelewa juu ya haki zetu kisheria ili tuweze kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza, MSLAC haki kwa usawa na maendeleo #sisinitanzania #mslac
ReplyDeleteTransparency, Accountability and inclusiveness
ReplyDelete#🇹🇿
#SSH
Utawala bora ndiyo msingi wa haki na usawa kwa jamii, pongezi kubwa kwa wizara kwa kuendele kutoa elimu hii kwa viongozi wetu.
ReplyDeleteUjenzi wa mfumo bora wa kutawala ni pamoja na mafunzo ya kuimarisha watendaji katika kujua na kufuata taratibu na sheria ili kuwa na msingi imara wa utawa bora.
ReplyDeletepongezi kwa serikali kwa kuona umuhumu wa kufikisha huduma hii mpaka level ya chini
ReplyDeleteWizara ya Katiba na Sheria imeweza kutambua haki za binadamu na kuhakikisha usalama wao#ssh
ReplyDelete#sisinitanzania #kaziiendelee #kazinaututunasongambele
ReplyDelete