MAENDELEO YA MJI WA MTUMBA DODOMA, KITUO KIKUU CHA OFISI ZA SERIKALI TANZANIA
Kufikia Mei 2024, jumla ya watumishi wa umma 25,039 na taasisi 65 tayari walikuwa wamehamia Dodoma na kuanza shughuli zao katika mji wa Mtumba. Ujenzi wa awamu ya pili wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi mbalimbali unaendelea, ambapo unatarajiwa kukamilika mwaka 2025.
Mnamo Julai 3, 2023, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba na kutoa maagizo kwamba ifikapo Oktoba mwaka huo, majengo yawe yamekamilika na kuwekwa samani, ili watumishi waanze kuyatumia ifikapo Januari 1, 2024.
Mradi wa ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba umeleta manufaa makubwa, ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi katika jiji la Dodoma. Aidha, Serikali imekuwa ikisisitiza matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini katika ujenzi huo, ili kuunga mkono viwanda vya ndani.
Maendeleo ya ujenzi wa mji wa Mtumba yamekuwa yakiridhisha, na Serikali inaendelea na jitihada za kukamilisha miradi iliyobaki kwa wakati ili kuhakikisha watumishi wa umma wanapata mazingira bora ya kufanyia kazi.
Ujenzi wa mji wa mtumba Dodoma umeleta mabadiliko Chanya ya mji wa Dodoma katika Sekta ya miundombinu, shughuri za kijamii na Uchumi. Hakika Dodoma inapendeza na kuvutia.
ReplyDelete#SisiNiTanzania
#HayaNdioMatokeoChanya+
#TanzaniaKwanza
#DrSSH
#Kaziiendelee
Mji wa Mitumba umeweza kuleta fursa kwa wananchi na mandolin katika Mkoa wa Dodoma kwa kukua kiuchumi na maendeleo katika jamii
ReplyDelete#ssh
#siondototena
#sisinitanzania