TANZANIA YAPAA KATIKA UZALISHAJI WA ASALI, NAFASI YA PILI BARANI AFRIKA NA FURSA MPYA SOKONI
Tanzania inazalisha wastani wa tani 33,276 za asali na tani 1,913 za nta kwa mwaka. Hata hivyo, kiwango hiki ni chini ya uwezo wa uzalishaji unaokadiriwa kufikia tani 138,000 za asali kwa mwaka.
Katika soko la kimataifa, Tanzania inashika nafasi ya pili barani Afrika kwa uzalishaji wa asali, ikitanguliwa na Ethiopia. Hata hivyo, ni asilimia tano tu ya asali inayozalishwa nchini ndiyo inauzwa nje ya nchi, huku asilimia 95 ikibaki katika masoko ya ndani.
Mnamo Agosti 2024, Tanzania ilisaini makubaliano na China kuruhusu uuzaji wa asali katika soko la China, ambalo lina mahitaji ya tani milioni 38 kwa mwaka. Hii ni fursa muhimu kwa wafugaji nyuki na wafanyabiashara wa asali nchini kuongeza uzalishaji na kuuza katika soko hilo kubwa.
Ili kuhakikisha ubora wa asali inayouzwa nje, serikali imezindua nembo ya asali ya Tanzania itakayotumika kuitambulisha bidhaa hiyo katika soko la dunia. Nembo hii inawahakikishia walaji kuwa bidhaa wanayotumia iko salama na inakidhi viwango vya ubora.
Pamoja na jitihada hizi, bado kuna changamoto katika kuongeza uzalishaji na mauzo ya asali nje ya nchi. Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafugaji nyuki kwa kutenga maeneo maalum ya kufugia nyuki na kujenga viwanda vya kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki katika mikoa mbalimbali.
Kwa ujumla, Tanzania ina nafasi nzuri katika uzalishaji wa asali barani Afrika na inaendelea kuchukua hatua za kuboresha uzalishaji na kuongeza ushiriki wake katika soko la kimataifa.
Kubwa ni Serikali yetu kutengeneza mazingira Rafiki katika uzalishaji wa Asali kupitia wazalishaji.Tuna uwezo wa kuwa sehemu ya Nchi zinazofanya vizuri pia Duniani katika uzalishaji wa asali nyingi na bora,tunaona mikoa ya kanda ya kati ilivo na uwezo wa kuzalisha asali kwa wingi,Serikali yetu Sikivu ione nnq bora zaidi na kuwaweza wazalishaji wetu wa asali #SisiNiTanzania #SSH #Kaziiendelee #MSLAC #KatibaNaSheria #Tanzania
ReplyDeleteHatua hii itasaidia kuongeza fursa kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi pia ni faida kwa taifa letu.
ReplyDelete#sisinitanzania #kaziindelee
Tunashukuru serikali ya Awamu ya Sita Chini Ya Dr Samia Suluhu Kwa kuboresha mazingira wezeshi ili kuweza kuongeza uzalishaji wa asali Nchini. Kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia njia za asili katika kuvuna asali.
ReplyDeleteNaipenda nchi yangu Tanzania #sisinitanzania#siondototena#kaziiendelee
ReplyDelete