MAFUNZO YA URAIA NA UTAWALA BORA YAIMARISHA UWEZO WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA KATIKA MIKOA YA IRINGA NA MARA

Katika juhudi za kuimarisha utawala bora na kukuza uelewa wa masuala ya uraia, Wizara ya Katiba na Sheria imeendesha mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa katika Halmashauri mbalimbali. Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kujenga upya misingi ya utawala bora kwa viongozi wa ngazi za mitaa.



Katika mkoa wa Iringa, mafunzo yalifanyika kwa:  

1. ⁠Manispaa ya Iringa  

2. ⁠Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  

3. ⁠Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo  

 

Jumla ya washiriki 110 walihudhuria mafunzo haya, wakiwemo Kamati za Usalama za Wilaya, Wakuu wa Idara wa Halmashauri, na Watendaji wa Kata. Mada zilizojadiliwa ni pamoja na 

- Uraia na Utawala Bora  

Lengo kuu lilikuwa kujenga uwezo wa viongozi katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kufuata misingi ya demokrasia.

 

Halmashauri ya Wilaya ya Rorya nayo ilijumuisha washiriki 38 waliogawanyika kama ifuatavyo 

- Watendaji wa Kata 26  

- Kamati ya Usalama ya Wilaya 5  

- Wataalamu wa Halmashauri 7  

 

MADA ZILIZOJADILIWA 

1. Haki na Wajibu  

2. Demokrasia na Utawala Bora  

3. Haki za Binadamu  

4. Madaraka ya Umma  

 


Mafunzo haya yalifunguliwa rasmi na Wakili wa Serikali Mkuu, Bi. Joyce Mushi, ambaye pia ni Mratibu wa Mafunzo haya.

 

Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo viongozi wa serikali za mitaa, hususan Kamati za Usalama, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi, ufanisi, na kujiamini huku wakizingatia misingi ya haki za binadamu na utawala bora. Kupitia mafunzo haya, viongozi wanatarajiwa kupata ujuzi wa kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kujenga jamii inayozingatia demokrasia na uwajibikaji.

 

Mafunzo haya yameanza katika mikoa ya Rukwa na sasa yanaendelea katika mikoa ya Mara, Morogoro, Iringa, na Songwe. Yanalenga kuhakikisha viongozi wanapokea mafunzo ya kina yatakayowasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Mafunzo haya ni kiini cha utekelezaji wa falsafa ya "Rebuild" ya Rais Samia Suluhu Hassan, ikilenga si tu kuboresha utendaji kazi wa viongozi wa serikali za mitaa, bali pia kuwajengea uelewa wa umuhimu wa kuhudumia wananchi kwa weledi na kwa kuzingatia haki na demokrasia.   

Comments

  1. Transparency, Accountability, Responsiveness, effectiveness and efficiency,🇹🇿

    ReplyDelete
  2. Watumishi wa umma ndio wasaidizi wa Rais, tukafanye kazi kwa bidii ili tusimuangushe kiongozi wetu #ssh #sisinitanzania #matokeochany

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JE, KAULI MBIU YA MHE. RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – 'KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE' INA MAANA GANI KWA MAENDELEO YA TANZANIA?

UMUHIMU WA ZIARA YA RAIS WA TFF KUKAGUA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU ARUSHA – KWA ULIMWENGU WA SOKA NA USTAWI WA TAIFA