MAENDELEO YA MJI WA MTUMBA DODOMA, KITUO KIKUU CHA OFISI ZA SERIKALI TANZANIA

Mji wa Mtumba, uliopo jijini Dodoma, ni eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya ofisi za Serikali ya Tanzania. Mpango wa kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma ulianza rasmi mwaka 2016, na tangu wakati huo, maendeleo makubwa yamefanyika katika ujenzi wa mji huu.

Kufikia Mei 2024, jumla ya watumishi wa umma 25,039 na taasisi 65 tayari walikuwa wamehamia Dodoma na kuanza shughuli zao katika mji wa Mtumba.  Ujenzi wa awamu ya pili wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi mbalimbali unaendelea, ambapo unatarajiwa kukamilika mwaka 2025.

 

Mnamo Julai 3, 2023, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba na kutoa maagizo kwamba ifikapo Oktoba mwaka huo, majengo yawe yamekamilika na kuwekwa samani, ili watumishi waanze kuyatumia ifikapo Januari 1, 2024. 


Mradi wa ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba umeleta manufaa makubwa, ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi katika jiji la Dodoma.  Aidha, Serikali imekuwa ikisisitiza matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini katika ujenzi huo, ili kuunga mkono viwanda vya ndani.

 

Maendeleo ya ujenzi wa mji wa Mtumba yamekuwa yakiridhisha, na Serikali inaendelea na jitihada za kukamilisha miradi iliyobaki kwa wakati ili kuhakikisha watumishi wa umma wanapata mazingira bora ya kufanyia kazi.

Comments

  1. Ujenzi wa mji wa mtumba Dodoma umeleta mabadiliko Chanya ya mji wa Dodoma katika Sekta ya miundombinu, shughuri za kijamii na Uchumi. Hakika Dodoma inapendeza na kuvutia.
    #SisiNiTanzania
    #HayaNdioMatokeoChanya+
    #TanzaniaKwanza
    #DrSSH
    #Kaziiendelee

    ReplyDelete
  2. Mji wa Mitumba umeweza kuleta fursa kwa wananchi na mandolin katika Mkoa wa Dodoma kwa kukua kiuchumi na maendeleo katika jamii
    #ssh
    #siondototena
    #sisinitanzania

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JE, KAULI MBIU YA MHE. RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – 'KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE' INA MAANA GANI KWA MAENDELEO YA TANZANIA?

UMUHIMU WA ZIARA YA RAIS WA TFF KUKAGUA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU ARUSHA – KWA ULIMWENGU WA SOKA NA USTAWI WA TAIFA