Kampuni ya Airplane Africa Limited (AAL), inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech, ilianzisha kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza ndege mwaka 2021 katika eneo la Mazimbu, mkoani Morogoro. Kiwanda hiki ni cha kwanza barani Afrika katika sekta hii.
Hadi kufikia Desemba 2024, AAL imefanikiwa kuunganisha na kutengeneza zaidi ya ndege tatu aina ya Skyleader 600, zenye uwezo wa kubeba abiria wawili hadi wanne. Ndege hizi zimeanza safari rasmi ndani na nje ya nchi, baada ya kupata cheti cha kuipasisha kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) mnamo Septemba 2024.
Kiwanda hiki kimeajiri mafundi wengi ambao ni wahitimu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), hivyo kuchangia katika kutoa uzoefu kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu, vyuo vya kati, na vyuo vya ufundi.
Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Uchukuzi, imeonyesha nia ya kusaidia sekta ya anga kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ili kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kama AAL. Hatua hii inalenga kuimarisha uwekezaji na kukuza teknolojia ya utengenezaji wa ndege nchini.
Kwa sasa, ndege zinazotengenezwa na AAL zinaweza kuuzwa katika nchi mbalimbali, na mipango ya baadaye ni kuunda ndege zenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya wawili.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kiwanda hiki na shughuli zake, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya Airplane Africa Limited.
Hatua Kubwa Ya usafiri wa Anga
JibuFutaKwa kweli Tanzania inasonga mbele. Miradi hii mikubwa ya maendeleo imekuwa chachu ya ajira lakini pia usafirishaji. Hii inaongeza kasi ya maendeleo kwa kiasi kikubwa. Hizi ni juhudi kubwa sana kwa nchi yetu chini ya Rais Dr Samia.
JibuFuta#ssh
#kaziendelee
#sisinitanzania
#matokechanya
#mslac
#wizarayakatibanasheria
Airplane Africa Limited ni mradi wa kimkakati unaoahidi kuleta mapinduzi makubwa katika viwanda na teknolojia Tanzania. Faida zake si tu kiuchumi bali pia kijamii, kwa kuwawezesha Watanzania kushiriki moja kwa moja katika sekta ya anga ya kimataifa.
JibuFutaTanzania tumeweza 🇹🇿
JibuFutaHaya yote yanatelekezwa ya serikali ya awamu ya 6 ya Dr. Samia Suluhu Hassan, kwa kweli Rais wetu ni mchapakazi na mpenda maendeleo #kaziiendelee #ssh #sisinitanzania #siondototena
JibuFutaTumethubutu na Tumeweza, Tanzania mbele daima. #nchiyangukwanza #sisinitanzania #kaziiendelee
JibuFutaPongezi kwa Mh.rais Hakika tunaiyona Kazi kubwa anayoifanya kwa kuleta maendeleo makubwa Nchini kwetu
JibuFuta#sisinitanzania
#matokeochanya
#SSH