KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA, WATENDAJI WA MIKOA NA HALMASHAURI ZA MKOA WA MARA WAPIGWA MSASA JUU YA UTAWALA BORA NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA


Wizara ya Katiba na  sheria imeanza kutoa  mafunzo ya utawala Bora  na Uraia kwa kamati za Usalama za Mikoa na Wilaya,wakuu wa idara mbalimbali za Halmashauri na watendaji wa Kata wilayani Rorya Mkoani Mara ili kuwakumbusha kuzingatia Mipaka katika utumishi wa umma na Misingi ya Utawala bora.

 


Akizungumza Wakati wa mafunzo hayo Wilayani Rorya Mkoani mara  Joyce mushi wakili wa serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia nimratibu wa mafunzo wa Elimu ya utawala Bora ambapo amesema Mafunzo hayo nimwendelezo wa mafunzo ambapo yalianzia Mkoa wa Rukwa huku walengwa wakuu wakiwa nikamati za Usalama watendaji wa kata na watumishi wa idara mbalimbali za Halmashauri.

 

Joyce alisema lengo la Mafunzo hayo nikuwakumbusha na kuwajengea uwezo washiriki ili waweze kuwa na Uelewa wakutekeleza majukumu Yao kwa kufata misingi ya utawala bora na haki za binadamu na demokrasia.

 


"Mafunzo hayo kutolewa niutekelezaji wa Falsafa ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan ya 4R- ya Ujenzi upya(Rebuilding) ambapo tunaamini tukimaliza Mafunzo haya washiriki wote watakuwa wamejengwa upya na Kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha kwa Wananchi"Joyce mushi wakili wa serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria"

 

Robhi Richard wambura Afisa mtendaji kata ya Roche nimiongoni mwa wanaufaika wa mafunzo hayo ambapo amemshukuru Rais DKT Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Katiba na Sheria alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwa chachu ya mabadiliko katika vituo vya kazi kutokana na kipindi cha Nyuma wengi wao walikuwa wanafanya kazi bila kuzingatia miiko na Mipaka yao yakazi.

 


Elimu ya Utawala bora na uraia kwa viongozi wa mamlaka za Serikali za mitaaa inaendelea katika Mkoa wa mara huku ikitarajiwa kufanyika katika Halmashauri zote za Mkoa huo wa Mara 

Comments

  1. Yote hayo ni kwaajili ya kuwajengea watumishi uwezo wa kufanya kazi kwa uadilifu, amani na utulivu. asante serilikali makini ya Dr. Samia #siondototena #ssh #sisinitanzania #kaziiendelee #matokeochanya

    ReplyDelete
  2. Mafunzo Haya yatawasaidia kufanya kazi kwa weledi na kuweza kutekeleza majukumu yao. Tunaishukuru serikali kwa kuweza kujali usalama wa wananchi wake
    #ssh
    #siondototena
    #matokeochanya

    ReplyDelete
  3. Tunaishukuru serikali chini ya rais wetu mpendwa DK.Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea elimu hii itakayowasaidia watumishi wa serikali za mitaa kufanya Kazi kwa weledi na ufanisi ili kuleta maendeleo kwa wananchi wake #sisinitanzania
    #matokeochanya #samiasuluhuhassan

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JE, KAULI MBIU YA MHE. RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – 'KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE' INA MAANA GANI KWA MAENDELEO YA TANZANIA?

UMUHIMU WA ZIARA YA RAIS WA TFF KUKAGUA UJENZI WA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU ARUSHA – KWA ULIMWENGU WA SOKA NA USTAWI WA TAIFA