Maelfu ya wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamefurika katika viwanja vya Tanganyika Pekasi, Kawe, jijini Dar es Salaam, kushuhudia uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Tukio hili limebeba taswira ya mshikamano na hamasa kubwa ya kisiasa huku viongozi wa kitaifa na wastaafu wakijumuika katika jukwaa moja.
Amani na Utulivu Wakitawala
Hadi sasa taifa linashuhudia hali ya amani na utulivu, jambo linaloendelea kudhihirisha msingi imara wa demokrasia ya Tanzania. Wananchi walijitokeza kwa wingi wakiwa na furaha, nyimbo na kauli mbiu za kuashiria mshikikano wa kisiasa na kijamii.
Umuhimu wa Tukio Kisheria na Kitaifa
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za Uchaguzi, kila chama kinaruhusiwa kufanya mikutano ya kampeni kwa heshima na amani. Uzinduzi huu wa CCM umekuwa ishara ya kuanza rasmi kwa mbio za kuelekea uchaguzi, huku ukizingatia misingi ya kidemokrasia.
Uwepo wa viongozi wote wa kitaifa na wastaafu umetoa uzito wa kipekee. Ni ishara ya mshikamano wa uongozi na heshima kwa taasisi za kisiasa. Watazamaji na wachambuzi wa siasa wanauona huu kuwa ni ujumbe wa umoja, mshikikano na mwendelezo wa falsafa ya amani Tanzania.
Mustakabali wa Taifa
Tanzania inaendelea kudumisha misingi ya uchaguzi wa huru na haki. Tukio la Kawe limeonesha wazi kuwa wananchi wapo tayari kushiriki kikamilifu katika mchakato huu. Mustakabali wa taifa letu unategemea zaidi mshikamano huu, kuheshimu sheria na kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa shindano la hoja badala ya chuki.
Kawe imekuwa kioo cha demokrasia na mshikamano wa kitaifa. Kadiri kampeni zinavyoendelea, macho yote yataelekezwa katika kudumisha amani, mshikamano na utulivu, ili taifa liendelee kusonga mbele kwa mshikamano na maendeleo.
Hii ni ishara kuwa wananchi wanaridhishwa na kazi Rais Samia pamoja na serikali anayoiongoza. Hii inadhihirisha imani yao juu ya kazi anayoifanya katika kuipatia Tanzania maendeleo
JibuFutaPongezi kwa serikali yetu kwa kuhakikisha Nchi yetu inaendelea kuwa na utulivu na amani hadi kufikia sasa..Ni imani yangu kua tutafanya uchaguzi kwa amani na utulivu kama ilivo desturi yetu watanzania
JibuFutaNina Imani kubwa sana na mh rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye kuiongoza nchi kwa miaka mitano tena,Mungu ajaalie nguvu na afya tele kipindi chote kampeni
JibuFutaKazi aliyofanya Dkt. Samia Watanzania tumeiona na tumeikubali. Amefanya mapinduzi makubwa sana katika kila sekta na kila halmashauri nchini. Zamani nilikua siipendi ccm, ila saizi nitampigia kura ya ndio Samia, na itakuwa mara yangu ya Kwanza kumpigia kura wa ccm. Hii si Mimi pekee, ni wengi sana kwenye mnyororo wangu wa marafiki watafanya hivyo.
JibuFutaWananchi tumekubali na tumeona kuna haja kubwa ya kumuunga mkono Mh Rais na kumpa nguvu kubwa itakayomtia moyo na kumpa msukumo zaidi katika kutuletea tena maendeleo mengine mengi katika miaka mingine mitano yaani 2025-2030
JibuFutaWatanzania tumemkubali Mama uwezo wake ni mkubwa Sana wa kuongoza na tumem verify kuwa anatosha sana oktobatunatiki ✅✅✅
JibuFutaWe are Tanzanians, we are ready for voting
JibuFuta