Alhamisi, 10 Julai 2025

MKOA WA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA NA RAFIKI YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Mkoa wa Dar es salaam umedhamiria kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji wa mizigo na watu kwa kujenga barabara bora ili kuufanya Mkoa huo uendelee kuwa kitovu cha uwekezaji na biashara na uendelee kuchangia kwenye pato la nchi kwa asilimia kubwa

Mkoa wa Dar es salaam umedhamiria kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji wa mizigo na watu kwa kujenga barabara bora ili kuufanya Mkoa huo uendelee kuwa kitovu cha uwekezaji na biashara na uendelee kuchangia kwenye pato la nchi kwa asilimia kubwa.



Akizungumza leo Julai 10, 2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Mkoa wa Dar es salaam yaani "Dar es salaam Day" kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sixtus Mapunda amesema Mkoa wa Dar es Salaam ni kitovu cha biashara na unachangia kwenye mapato ya nchi kwa asilimia 17 hivyo Mkoa unaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na madaraja kwa ajili ya usafirishaji, ambapo amesema Mkoa huo unafursa na maeneo mengi kwa ajili ya uwekezaji na biashara kwenye kila wilaya na kwamba ubora wa Mkoa huo unachagizwa na kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuimarisha Bandari,Usafiri wa reli ya kisasa,uwanja wa ndege pamoja uwepo wa huduma bora za umeme na maji.



Aidha Mhe Mapunda ametoa mchanganuo wa maeneo ya uwekezaji kwa kila wilaya ambapo Wilaya ya Temeke ni maeneo 17,kinondoni maeneo 29 Jiji la Dar es Salaam maeneo 9, kigamboni maeneo 27 na ubungo maeneo maeneo 6 kwa ajili ya uwekezaji.

Kwa upande waKatibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bwana Abdul Mhite amesema katika kuimarisha shughuli za biashara na uwekezaji Mkoa huo umekuwa na mikakati mbalimbali ikiwemo kuanzisha mfumo wa biashara saa 24 pamoja na kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wafanyabiashara ambapo zaidi ya vikundi 2000 tayari vimepatiwa mikopo



Maadhimisho ya siku ya Mkoa wa Dar es salaam yamefanyika kwenye viwanja vya SABASABA huku yakijielekeza kwenye mkakati wa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA

Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...