Jumanne, 27 Mei 2025
MWENGE WA UHURU WAZINDUA NEEMA YA MAJI TANDAHIMBA – VIJIJI 5 KUFAIDIKA
Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba, Falaura Kikusa alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya Programu Maalumu ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inayolenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama.
“Mradi huu ni mkakati maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kupunguza adha ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hii muhimu. Utekelezaji wake ulianza Mei 2024 na unatarajiwa kukamilika Juni 2025 kutokana na changamoto mbalimbali, licha ya mpango wa awali kumalizika Disemba 2024,” alisema Kikusa.Kikusa alieleza kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 76, ambapo miundombinu ya maji ikiwemo usimikaji wa matanki ya lita 10,000 imekamilika katika vijiji viwili vya Mivanga na Lyenje, huku usimikaji wa pampu na mifumo ya nishati ya jua ukiwa umefanyika katika vijiji vya Mivanga, Lyenje, Dinduma na Mchangani.
Kwa mujibu wa Kikusa, gharama ya kisima kimoja ni Shilingi 90,500,000 na hadi sasa Shilingi 124,106,686.40 kati ya fedha zilizotengwa tayari zimelipwa. Fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo mpango wa Lipa kwa Matokeo, Mfuko wa Taifa wa Maji na michango ya wadau wa maendeleo.
Aidha, alisema mradi huo umetoa ajira za muda mfupi kwa wananchi wa maeneo husika wakiwemo mafundi, wapishi, na madereva, huku pia ukichochea maendeleo ya kilimo na kusaidia kupunguza magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara.
Katika kijiji cha Mivanga, kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha maji lita 372,000 kwa siku. Wananchi wa vijiji hivyo wametoa maeneo ya ujenzi wa visima hivyo bila fidia, yenye thamani ya takriban Shilingi 2,500,000.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed ameishukuru serikali kupitia RUWASA kwa kutekeleza mradi huo muhimu na kusisitiza kuwa umeleta afueni kubwa kwa wananchi waliokuwa wanatumia gharama kubwa na muda mwingi kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujali ustawi wa wananchi wa Tandahimba na kuwataka wakazi wa vijiji walionufaika na mradi huo kushirikiana na serikali kuutunza ili udumu kwa muda mrefu.
Mkazi wa kijiji cha Mivanga, Bi. Asha Seleman alisema mradi huo umesaidia kupunguza gharama za maisha kwa wakazi wa kijiji hicho kwani hapo awali walikuwa wananunua ndoo moja ya maji ya lita 20 kwa Shilingi 1,000.
MUHAS KUANZA MAFUNZO MAALUM KWA GYM INSTRUCTORS ILI KUBORESHA USALAMA WA MAZOEZI KWA WAGONJWA
CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kuanza kutoa mafunzo maalum ya kitaalamu kwa wakufunzi wa mazoezi ya viungo (gym instructors) na wasimamizi wa kumbi za mazoezi (fitness managers),ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wateja wanaopelekwa kufanya mazoezi kwa sababu za kitabibu.
Akizungumza leo Mei21,2025 wakati wa uzinduzi wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa afya ya moyo bila malipo katika Kampasi ya MUHAS Mloganzila,Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Appolinary Kamuhabwa moja amesema mpango huo unalenga kulinganisha huduma za mazoezi ya viungo ya viwango vya kitaifa vya afya.
“Uzoefu unaonesha kuwa watu wengi huanza mazoezi bila ushauri wa kitabibu, jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa afya hususani moyo,” amesema Profesa Kamuhabwa.
Ameongeza,“Lengo letu ni kuwajengea uwezo waendeshaji wa kumbi za mazoezi ili waweze kutoa huduma kwa kufuata taratibu za kitaalamu za afya,”
Ameonya suala la jamii kufanya mazoezi bila usimamizi wa kitabibu kunaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha ghafla kwa watu wenye magonjwa ya moyo au matatizo mengine ya kiafya yaliyofichika.
Profesa Kamuhabwa amesema kama sehemu ya mpango huo, MUHAS itazindua kituo kipya cha mazoezi ya viungo mapema wiki hii, ambacho kitakuwa kinatoa vyeti vya mazoezi kama ilivyo kwa dawa zinazotolewa kwa agizo la daktari.
Amesema mafunzo hayo pamoja na uanzishaji wa gym hiyo ni sehemu ya jitihada za kuboresha kiwango cha huduma za mazoezi ya viungo nchini na kupunguza hatari za kiafya kutokana na mazoezi yasiyo na miongozo ya kitaalamu.
Akizungumzia kambi ya uchunguzi inayoendelea, Profesa Kamuhabwa amesema shughuli mbalimbali zinazofanyika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya Kituo cha Umahiri cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni pamoja na huduma za magonjwa ya moyo, kinga na tiba kwa wale watabainika kuwa na matatizo ya moyo.
Kwa upande wake, mtaalamu wa fiziolojia Irine Mngolokolo,amesema gym hiyo mpya imeundwa mahsusi kwa ajili ya watu wenye changamoto za kiafya.
Irene ambaye pia ni msaidizi wa kufundisha katika kituo hicho amesisitiza umuhimu wa kuanza mazoezi kwa mpango maalum uliopangwa na mtaalamu, iwe ni ya aerobic au anaerobic, kulingana na mahitaji ya mhusika.
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Emmanuel Balandya, amesema kuwa mafunzo ya wataalamu wa afya ya moyo ni moja ya vipaumbele vikuu vya MUHAS.
Ijumaa, 23 Mei 2025
Alhamisi, 22 Mei 2025
VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA
Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...

-
Kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan –"Kazi na Utu Tunasonga Mbele" – ni dira ya maende...
-
MAFUNZO YA WAJUMBE WA KAMATI YA USALAMA KUHUSU ELIMU YA URAIA NA UTAWALA BORA YANAYORATIBIWA NA WIZARA YA SHERIA NA KATIBA YANAFANYIKA MKO...
-
Ziara ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia , ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu...