Alhamisi, 24 Aprili 2025

VIJANA WA KILOSA WANG’ARA KUPITIA KILIMO CHA ALIZETI – MVIHAWIKI YAWAINUA KIUCHUMI

Vijana 40 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wameungana kupitia Mtandao wa Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (MVIHAWIKI) kuanzisha shamba la alizeti lenye jumla ya ekari 20, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwawezesha kiuchumi. Kati ya vijana hao, 29 ni wanaume na 11 ni wanawake.

Maandalizi ya shamba hilo yamegharimu shilingi milioni 3.72 zilizotolewa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri hiyo, chini ya Mpango wa Maendeleo ya Vijana wa Taifa wa mwaka 2007 na Mkakati wa utekelezaji wa miaka 10 (2024–2034).

Mradi huu unaunga mkono maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia program ya Build a Better Tomorrow (BBT), inayolenga kuwainua vijana kiuchumi kupitia sekta ya kilimo.

Maoni 5 :

  1. Idara ya kilimo ni idara nyeti na serikali ikiendelea kuwekeza ngu huku na vijana kuamua na masoko kutengenezwa vizuri umaskini utakuwa ni ndoto kwa taifa letu

    JibuFuta
  2. Kujihusisha na kilimo kunaweza kuwapa vijana ujasiri na uwezo wa kujitegemea kwani Alizeti ni zao linaloweza kuleta faida kubwa kutokana na mahitaji yake sokoni #ssh #mslac #SisiNiTanzania #NaipendaNchiYangu #matokeochanya #katibaNaSheria #NchiYanguKwanza

    JibuFuta
  3. Build better tomorrow ni mpango mkakati unaenda kuwainua vijana kiuchumi kupitia kilimo

    JibuFuta
  4. Taifa lenye vijana wanaolalamika kila Kukicha haliwezi kusonga Mbele. Kwa kila tulichonacho lazima tukitumie tuondokane na Tatizo la ajira. Hawa Ndio vijana wanaoliheshimisha Taifa letu Kwa vitendo πŸ‘πŸ‘πŸ‘
    Kazi Na Utu, Tunasonga Mbele πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
    #SisiNiTanzania
    #Matokeochanya
    #MsLAC

    JibuFuta
  5. Kazi na utu tunasonga mbele #sisinitanzania #kaziiendelee #katiba nasheria # matokeochanya

    JibuFuta

VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA

Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...