Vijana 10 wa Kimashale Wapambana na Umaskini kwa Ubunifu wa Uchomeleaji Vyuma

Gairo, Morogoro – Katika kijiji kidogo cha Kimashale, kata ya Chakwale wilayani Gairo, vijana 10 wameandika historia mpya ya matumaini, wakichukua hatua ya kishujaa kupambana na adui mkubwa wa maendeleo – umaskini. Kwa mtaji wa Shilingi milioni 3 tu, walizindua rasmi shughuli za uchomeleaji vyuma mwezi Machi 2023, wakiongozwa na ndoto, juhudi, mshikamano na maono ya kuona mabadiliko katika jamii yao. Kupitia uhitaji mkubwa wa huduma ya uchomeleaji katika kijiji chao na maeneo ya jirani, kikundi hiki kilitambua fursa ya kipekee na kuichangamkia kwa ubunifu. Kwa kuonesha uwajibikaji, weledi na mipango thabiti ya biashara, walifuzu kupata mkopo wa Shilingi milioni 15 kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri – fedha maalum zinazotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu – kwa riba nafuu ya asilimia 4 tu. Mafanikio yao hayakuchelewa kuonekana. Kupitia mkopo huo, walinunua vifaa vya kisasa vya uchomeleaji ambavyo vimeongeza tija na ufanisi wa kazi zao. Ubora wa bidhaa ul...