SERIKALI YAREKEBISHA KANUNI ZA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI ILI KURAHISISHA HUDUMA.
Dodoma, Tanzania – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imerekebisha Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2019 na kutangaza kanuni mpya za mwaka 2023 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kubadilisha fedha za kigeni nchini.
Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Hamad Hassan Chande, alitoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni, Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, aliyehoji hatua zilizochukuliwa na serikali ili kuhakikisha huduma za kubadilisha fedha zinapatikana kwa urahisi karibu na hoteli za kitalii Zanzibar.
Mheshimiwa Chande alisema kuwa marekebisho hayo yameleta mafanikio makubwa, ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Zanzibar kutoka maduka manne (4) yenye matawi kumi na moja (11) hadi maduka kumi na tano (15) yenye matawi thelathini na tano (35).
Aidha, alieleza kuwa mabadiliko hayo yalitangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 42 la Oktoba 2023, ambapo hoteli zote zenye hadhi ya nyota tatu au zaidi sasa zina fursa ya kuomba leseni za kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kupitia Dirisha la Daraja C. Hatua hii inalenga kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma hizo kwa watalii na wageni wa kimataifa.
Mheshimiwa Chande alifafanua zaidi kuwa kanuni mpya zimeanzisha madaraja matatu (A, B, na C) kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, huku masharti ya mtaji wa kuanzisha maduka hayo yakiwa yamepunguzwa ili kurahisisha upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuimarisha sekta ya utalii na biashara nchini kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi na ufanisi zaidi.
#ssh #tanzaniayangu #matokeochanya #sisinitanzania #mslac #kaziiendelee
ReplyDeleteHaya ni matokeo chanya chini ya Amiri Jeshi Mkuu Dr. Samia Suluhu Hassan #sisinitanzania #mslac #matokeochanya #siondototena
ReplyDeleteMatokeo chanya #ssh #sisinitanzania #katibanasheria #Mslac #kaziiendelee
ReplyDelete