TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 73 WA BARAZA LA KIMATAIFA LA VIWANJA VYA NDEGE KANDA YA AFRIKA
Tanzania inajivunia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege Kanda ya Afrika (ACI Africa), tukio litakalojikita katika kuendeleza maslahi ya pamoja ya viwanja vya ndege na kukuza ubora wa kitaaluma ili kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya usafiri wa anga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema maandalizi ya mkutano huo yanakwenda vizuri kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Mkutano huo unatarajiwa kuwahusisha zaidi ya wajumbe 400, wakiwemo wawakilishi kutoka nchi wanachama 75 zenye viwanja vya ndege zaidi ya 265 katika nchi 54 za Afrika, pamoja na washiriki 59 wa sekta ya usafiri wa anga.
Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, mkutano huo pia utajumuisha mikutano ya bodi, kamati tendaji, pamoja na maonyesho ya viwanja vya ndege mbalimbali. “Hii ni fursa muhimu kwa nchi yetu kujitangaza, hasa kwa vivutio vyetu vya kiutalii,” alisema Waziri Mbarawa.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuelekea Wakati Ujao Bora wa Kijani: Kutumia Usafiri wa Anga Endelevu na Utalii wa Ustawi wa Kiuchumi” Tukio hili litaangazia hatua za maendeleo endelevu katika sekta ya usafiri wa anga huku likionyesha dhamira ya Tanzania katika utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Abdul Mombokaleo, amesema mamlaka hiyo imejipanga kuboresha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika viwanja vyote vya ndege nchini. Aidha, alisema miradi ya kibiashara na urasimishaji wa hati miliki za viwanja vya ndege itaimarishwa zaidi kupitia mkutano huo.
“Mkutano huu ni tukio kubwa, na mamlaka yetu ni sekta mtambuka yenye umuhimu mkubwa. Kufanyika kwa mkutano huu jijini Arusha kunatoa fursa ya kipekee ya kuitangaza Tanzania, hususan vivutio vyetu vya kiutalii,” alisema Bw. Mombokaleo.
Mkutano huu unatarajiwa kuimarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya kimataifa ya sekta ya anga, huku ukitoa mchango muhimu katika maendeleo ya uchumi na utalii wa nchi.
Uongozi Imara wa #SSH unafanya Tanzania yetu iaminike kimataifa #sisinitanzania na haya ni #matokeochanya
ReplyDeleteTanzania inaendelea kuwa sehemu muhimu katika kutoa mchango wake kimataifa kutokana na misingi ya aman na upendo, Arusha ni mjii wenye vivutio vikubwa Duniani. Mkutano huu ukawe fusa katika kutangaza utalii hapa Nchini.
ReplyDelete#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Tanzania inaendelea kuimarika chini ya uongozi wa awamu ya sita, Dr Samia Suluhu Hassan. Na tunaamini kuwa mkutano huu wa 73 wa Baraza la kimataifa la viwanja vya ndege Afrika utakaofanyika jijini Arusha April 24-30 utaleta matokeo chanya na makubwa zaidi kwa nchi yetu πΉπΏπΉπΏ #sisinitanzania #sisindiowanjenziwataifaletu #matokeochanya #SSH #Kaziiendeleee
ReplyDeleteUpendo, amani na utulivu unaoimarishwa na mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan pamoja na serekali yake ndio unafanya kwa kiasi Kikubw Tanzania kuwa mwenyekiti wa mkutano kama hii ya kimataifa mkutano huu wa 73 wa baraza la kimataifa ukawe na matokeo chanya Tanzania. #SSH #matokeochanya #SISINITANZANIA
ReplyDelete