UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA INAYOHUSIKA NA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NASHERIA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi leo tarehe 04 Desemba, 2024 amekutana na kufanya kikao na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Imani Aboud aliyeambatana na ujumbe kutoka Mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba, jijini Dodoma viongozi hao wamejadili kuhusu nafasi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika kusimamia na kulinda Haki za Binadamu na Watu wa Afrika.
Waziri Kabudi amesema yapo maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa zaidi katika Mahakama ili kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo ambapo pia wamejadili changamoto zinazoikabili sekta ya Mahakama ambapo wamekubaliana kuendeleza majadiliano kwa ajili ya kuzifanyia kazi changamoto hizo ili kuiwezesha Mahakama kutimiza majukumu yake ambayo imepewa chini ya Mkataba wa kuanzishwa kwa Mahakama hiyo.
Viongozi hao pia wamepitia mambo ambayo Tanzania inawajibu wa kuyatekeleza chini ya Mkataba wa kuwa Mwenyeji wa Mahakama hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Kabudi Kabudi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo kubwa la Mahakama Afrika, ambapo amesema kuwa mambo mengi yanayofanywa katika Mahakama hiyo yanaendana na utekelezaji wa falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Kuboresha na Kujenga upya.
Waziri Kabudi amesema kuwa kwa sasa Wizara inaandaa Muswada wa utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai na katika kufanya hivyo miongoni mwa nyaraka zitakazotumika ni pamoja na maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Vyombo vinavyoshughurikia masuala ya haki na Usawa vikifanya kazi Kwa pamoja kuboresha namna ya Utoaji huduma na hujenga Imani Kwa Wananchi katika haki na Usawa mbele ya Sheria.
JibuFutaKwa kutambuliwa katika katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Haki za binadam,Basi kama Nchi tunapaswa kuzingatia sana hilo..Ni matumaini yetu kua tutaendelea kuheshimu ma kutambua haki za binadam kama ilivyo ainishwa katika katiba yetu.
JibuFuta#SisiNiTanzania #SSH #Tanzania #MSLAC #Katibanasheria
Tanzania imara 🇹🇿
JibuFuta#SisiNiTanzania
#matokeochanya
#SSH