Ijumaa, 27 Desemba 2024

UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA, TAKWIMU NA MAFANIKIO YA MIAKA MITATU (2021-2023)

Tanzania imekuwa ikishuhudia ukuaji thabiti wa uchumi kwa miaka kadhaa. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), ukuaji wa uchumi wa Tanzania ulikuwa kama ifuatavyo:  

 

2021, Uchumi ulikua kwa asilimia 4.9, licha ya changamoto za janga la COVID-19. 

 

2022, Ukuaji uliongezeka hadi asilimia 5.3, ukichochewa na miradi mikubwa ya maendeleo kama SGR, Mwalimu Nyerere Hydropower, na EACOP.  


2023, Uchumi ulionyesha kasi zaidi kwa ukuaji wa asilimia 5.8, ukihamasishwa na ongezeko la uwekezaji wa ndani na nje.  

 

Sekta zilizoongoza katika ukuaji wa uchumi ni pamoja na.. 

Kilimo: Huchangia takriban asilimia 26.9  ya Pato la Taifa (GDP).  

 

Ujenz: Ulichangia kwa asilimia 14.3 kutokana na miradi mikubwa ya miundombinu. 

 

Utalii: Mapato ya utalii yalifikia Dola za Marekani 2.6 bilioni mwaka 2023, yakirejea kutoka athari za COVID-19.  

 

Ukuaji huu umeimarisha maisha ya Watanzania, kupunguza umaskini, na kuimarisha huduma za msingi kama elimu, afya, na maji safi.

Maoni 1 :

  1. Maendeleo Haya ni ishara tosha katika maendeleo endelevu yenye tija Kwa Wananchi katika upatikanaji wa huduma za jamii kama vile barabara vijijini na mijini, zahanati Bora, maji safi na fursa za kibiashara kuongezeka kutokana na ukuaji wa kilimo.
    #SisiNiTanzania
    #HayaNdioMatokeoChanya+
    #MSLAC
    #DrSSH
    #Kaziiendelee

    JibuFuta

Vijana wa Mwanza Waandika Historia Mpya ya Maendeleo

  Leo Februari 19,2026 ni siku ya kipekee kwa vijana wa Mwanza. Ni mwanzo wa enzi mpya—enzi ya matumaini, ubunifu na mafanikio. Uzinduzi wa ...