Jumapili, 1 Desemba 2024

TUMIA NJIA SAHIHI, KUTOKOMEZA UKIMWI: 

Maendeleo ya Jamii Musoma Yawagusa Yatima, Wazee, na Walemavu  Manispaa ya Musoma Yaadhimisha Siku ya UKIMWI kwa Upendo na Elimu 




Katika kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani, Maafisa wa Maendeleo ya Jamii kutoka Dawati la Msaada wa Kisheria Manispaa ya Musoma wameonyesha mshikamano wa kipekee kwa kutembelea makundi yenye uhitaji maalum, ikiwemo yatima, wazee, na walemavu. Katika tukio hilo, misaada muhimu imetolewa kwa wahitaji ikiwa ni sehemu ya kujenga jamii yenye mshikamano na matumaini. 





Zaidi ya kutoa misaada, Idara ya Maendeleo ya Jamii ilitumia fursa hiyo kuelimisha wananchi kuhusu msaada wa kisheria, majukumu ya Dawati la Msaada wa Kisheria, na kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign. Hatua hizi zinakusudia sio tu kuboresha maisha ya wananchi, bali pia kutoa mwanga kuhusu haki zao za kisheria na namna ya kuzifikia.  





Kaulimbiu ya mwaka huu, "Tumia Njia Sahihi, Kutokomeza UKIMWI," inasisitiza umuhimu wa kuchukua hatua zinazozingatia afya, haki, na ushirikiano katika mapambano dhidi ya janga hili.  

Maoni 2 :

  1. Ni mwangaza Kwa jamii Ndio kitu kimefanyika na maafisa wa Dawati la Msaada wa Kisheria katika siku hii ya maadhimisho ya UKIMWI Dunia. Hongera kwao na Kwa jamii kupata Elimu ya msaada wa Kisheria.

    JibuFuta
  2. Hongera sana Kwa Dawati la msaada wa kisheria na hasa katika siku hii ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani, pongezi ziende kwa serikali ya awamu ya sita Kwa kujali wananchi wake

    JibuFuta

VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA

Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...