RAIS SAMIA ASEMA YA MOYONI
"Je, unakubaliana na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba Tanzania si nchi masikini, bali ni matajiri wa rasilimali lakini tuna changamoto za kuzitumia kwa ufanisi? Jadili kwa kutoa mifano halisi kuhusu rasilimali zetu na jinsi zinavyoweza kuboresha maisha ya kila Mtanzania."
JADILI
Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan inaonyesha mtazamo kwamba umasikini ni tafsiri inayotegemea vigezo vinavyotumika kuutathmini. Rais anaweka msisitizo kwamba Tanzania si masikini, bali ni nchi tajiri yenye rasilimali nyingi ambazo zinaweza kutumiwa kuboresha maisha ya watu wake.
Naunga mkono hoja Sisi Tanzania sio masikini tuna rasilimali Nyingi za muhimu ila tunachangamoto ndogondogo ambazo tukizipatia ufumbuzi tutapiga hatua kubwa,
Mfano katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Kilimanjaro tuna zao la Mkonge ambalo ni zao muhimu sana #SisiNiTanzania #SSH
Tanzania ni nchi ambayo tukitumia vizur rasilimali zetu tunaweza kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo,kwa mfano tuna eneo(ardhi) kubwa ambalo liko waz ,tukilitumia kwa uwekezaji wa miradi mbalimbali au viwanda vitaweza kuchangia pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi
Fursa za Kiuchumi
Viwanda na Biashara
Rasilimali za madini, kilimo, na uvuvi zinaweza kutumika kama malighafi kwa viwanda vya ndani, ambavyo vinaweza kukuza ajira na kuongeza thamani ya bidhaa.
Sekta ya biashara ya kimataifa inakua, hasa kupitia bandari za Dar es Salaam, Tanga, na Mtwara, zinazohudumia nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kama Zambia, DRC, na Malawi.
Tanzania imewekeza katika miradi mikubwa ya miundombinu, mfano:Reli ya SGR (Standard Gauge Railway): Itarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kati ya Tanzania na nchi jirani.
Barabara: Maendeleo ya mtandao wa barabara yanaharakisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na madini hadi masoko.
Umeme: Mradi wa Mwalimu Nyerere Hydropower na uwekezaji katika nishati mbadala kama upepo na jua vinaimarisha upatikanaji wa umeme.
Idadi Kubwa ya vijana Tanzania inatoa tumaini la Nguvu kazi kwenye uzalishaji katika Sekta za kiuchumi kama vile kilimo, Viwanda,na biashara. Nguvu kazi zikielekezwa katika uzalishaji ujenga Uchumi wa Nchi husika.
ReplyDelete#SisiNiTanzania
#HayaNdioMatokeoChanya+
#SisiNiTanzania
#MSLAC
This comment has been removed by the author.
DeleteManeno ya Dr SAMIA ni ukweli mtupu na usiopingika sisi ni matajiri na nchi yetu haina umasikini. Ni nukuu kwake kusema neno "umasikini ni tafsiri tuu"
ReplyDeleteRasilimali zetu kama maharishi ya finding yenye mandarin kubwa nyingi, MAZIWA MAKUU YALIYO TUZUNGUKA, Ni utajiri mkubwa:
Madini adimu duniani ya Tanzanite na madini yanayopatikana katika migodi yetu mingine ya kila aina, misitu mashamba makubwa ,na mifugo tulionayo ni utajiri mkubwa sana na kila mtazania anaishi kwa amani na habughudhiwi akitoka scheme moja kwenda nyingine kutafuta ama kustarehe huo ni utajiri mkubwa
Zaidi tunacho kuwa nacho ni changamoto ndogo ndogo
#SSH
ReplyDelete#SIS NI TANZANIA
#KAZI IENDELEE
Ninakubaliana na Rais Samia kwamba Tanzania si masikini bali ina rasilimali nyingi, kama madini, gesi, ardhi, na utalii. Changamoto zipo katika kuzitumia kwa ufanisi. Kwa mfano, sekta ya madini na kilimo zinaweza kuimarisha uchumi zaidi tukidhibiti upotevu na kuongeza thamani ya bidhaa.
ReplyDeleteChini ya uongozi wa Rais Samia, hatua zimeanza kuchukuliwa, na tukiendelea kushirikiana, maisha ya kila Mtanzania yanaweza kuboreka. Tanzania ni nchi yenye fursa kubwa!
Hakika Nchi yetu imebarikiwa sana kwa utajiri wa rasilimali mbalimbali. Tuna madini ya kutosha, mbuga za utalii na mlima kilimanjaro, ardhi kubwa na yenye rotuba, bandari za ukanda wa pwani ya bahari ya hindi, maziwa, mito na bahari,gesi na mafuta, pamoja na vingine vingi.
ReplyDeleteTukipata watu waadilifu na wazalendo wanaoweza kutumia rasilimali zetu hizi kwa uaminifu mkubwa, hakika tutapiga hatua kubwa kimaendeleo kwani rasilimali hizo zitanufaisha Taifa letu.
#SisiniTanzania tuijenge nchi yetu
#Matokeochanya tutayaona tukiwa waadilifu
#SSH
#kaziiendelee
Ni kweli kabisa Rais #DrSSH alivosema mfano sector ya madini ni rasilimali kubwa sana ambayo kama itasimamiwa vizuri na kuhakikisha hakuna utoroshaji holela wa madini inasaidia kwa kiwango kikubwa kukua kwa sector ya uchumi hapa nchi kwetu maana tuna madini ya kila aina mfani Tanzanite, Dhahabu, Almasi, nk,na kupitia sector hii vijana wengi wanajipatia ajira na kuondokana na umasikini. #sisinitanzania
ReplyDelete#SSH
ReplyDeleteNi kweli kabisa Tanzania ni nchi tajiri sana kwa kuwa tumebarikiwa rasili mali nyingi kma rasili mali watu ambao kwa idadi kubwa ni vijana wanaochangia nguvu kazi ya taifa pia tumejaaliwa mali asili bahari, mito na maziwa makubwa yanayochangia ukuaji wa uchumi wetu kwa kiasi kikubwa
#ssh
#hayandiomatokeochanya#sisiniTanzania
#MSLAC
Kiukweli kabisa, Tanzania sio nchi maskini ispokuwa ni fikra ambazo zipo akilini mwa watanzania kwamba hili linanihusu hili halinihusu. Tuna rasilimali nyingi kubwa kabisa ikiwa ardhi yenye rutuba. Sehemu ya ardhi ambayo imekwisha tumika haizidi hata nusu ya eneo zima la Tanzania. Lakini pia tuna madini, vivutio vya utalii na kubwa kuliko yote ni amani tunayojivunia kuwa nayo. Hivyo Tanzania sio Nchi maskini na mimi ninakubaliana na Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan.
ReplyDeleteNinakubaliana na Rais Samia kwamba Tanzania si masikini bali ina rasilimali nyingi, kama madini, gesi, ardhi, na utalii. Changamoto zipo katika kuzitumia kwa ufanisi. Kwa mfano, sekta ya madini na kilimo zinaweza kuimarisha uchumi zaidi tukidhibiti upotevu na kuongeza thamani ya bidhaa.
ReplyDelete#SSH
Nakubali, kwani Tanzania ina rasilimali nyingi za kipekee ambazo, kama zitatumiwa kwa ufanisi, zinaweza kuboresha maisha ya wananchi
ReplyDelete1. Madini na Maliasili:
Tanzania ina madini mengi kama dhahabu, almasi, tanzanite, na madini mengine yenye thamani kubwa duniani. Kwa mfano, madini ya tanzanite yanapatikana Tanzania pekee, na yanaweza kuingiza pato kubwa kama yatasimamiwa vyema na kuepuka uvujaji wa mapato kupitia magendo
2. Ardhi na Kilimo:
Tanzania ina ardhi kubwa na yenye rutuba inayofaa kwa kilimo na ufugaji
3. . Maliasili za Utalii:
Tanzania ina vivutio vya kitalii vya kimataifa, kama Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti, na visiwa vya Zanzibar. Na recently tulipokea award ya African's leading national parks
Ni ukweli usiopingika Tanzania si nchi maskini kwasababu Raslimali zote za thamani zinapatikana Tanzania, huo ni mtaji kwanza.
ReplyDeleteLakini kuzitumia Raslimali hizi kwa maslahi mapana ya Taifa letu na Taifa lisonge mbele tunamhitaji Rais mwadilifu ambaye ni Dkt Samia Suluh Hassan na viongozi waadilifu na wazalendo wa kweli ili wafanye kazi na Rais kwa kunia mamoja ili tuufurahie utajiri wetu Tanzania. ni ukweli usiopingika Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya kazi muda mfupi lakini matokeo yake ni makubwa sana. ninachotaka kushauri ni kwamba watanzania wenzangu mnapopewa nafasi kulitumikia Taifa fanyeni kazi kwa bidii.Kama umekabidhiwa kusimamia eneo Fulani fanya kwa uaminifu na moyo wa kuipenda nchi yako ili Dunia ijue jinsi Tanzania ni Taifa lililobarikiwa na Mungu.
#sisinitanzania
#RaisDktSamiaSuluhuHassan
#sisindiowajenziwatanzaniayet
Nakubali kwa kauli ya Rais wetu dr. Samia Suluhu Hassan kwamba sisi sio maskini kwasababu tunazo rasilimali nyingi za asili ambazo niutajiri kwetu...ukiangalia kweny katiba kuna kanuni ya utunzaji rasilimali zetu kwa maendeleo ya uchumi wa wananchi na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo nijukumu letu sisi na viongozi wetu kizitunza rasilimali zetu za asili maana nikwamanufaa yetu na vizaza ijavyo #sisinitanzania #nchiyangukwanza
ReplyDeleteNi sahihi kabisa kua Tanzania tuna rasilimali za kutosha kama asemavyo mhe Rais.Kilichokosekana ni matumizi sahihi ya hizo rasilimali tulizonazo mfano.Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 barani Africa zinazochimba madini ya Dhahabu kwa wingi lakini pia ni Ncji inayochimba Madini ya Tanzanite,hivyo basi ni muhimu kutafuta namna bora ya kuweza kutumia vema hizi Rasilimali zetu kwa maendeleo ya Nchi na watu wake.
ReplyDelete#SisiNiTanzania
#SSH
#Tanzania
Tanzania si Nchi Masikini Bali ni Matajiri wa rasilimali na utajiri unachangiwa vyanzo tulivyo navyo kama vile Madini, Mbuga za wanyama,Bwawa kubwa la kufulia umeme la mwalim Nyerere, Usafirishaji na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo mikakati ya kukabiliana na changamoto za uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya na elimu.
ReplyDeleteNakubaliana na kauli ya Dr Samia Tanzania sio nchi masikini tumebarikiwa rasilimali za kutosha ambapo tukizitumia kwa usahihi zitainua pato la nchi yetu ,miongoni mwa rasilimali hizo :-
ReplyDelete- Madini:Tanzania ina akiba kubwa ya madini kama dhahabu, almasi, tanzanite, na nickel. madini haya yanapouzwa nje ya nchi inachangia asilimia kubwa ya mapato ya nchi.
- Kilimo:Nchi ina ardhi nzuri kwa kilimo cha mazao kama kahawa, chai, pamba, na korosho. Sekta hii inatoa ajira kwa watu wengi na ni muhimu kwa uchumi wa nchi na inaimarisha uhusiano wa nchi yetu na mataifa mengine kibiashara
Utalii - Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Serengeti, Visiwa vya Zanzibar na Ziwa Nyasa. Utalii unachangia sana kwenye pato la taifa na unatoa fursa za ajira.
Nishati - Tanzania ina rasilimali za nishati, ikiwemo gesi asilia, ambayo inaweza kutumika kuzalisha umeme na kuimarisha uchumi.
Ingawa Tanzania ina rasilimali nyingi, kuna changamoto kadhaa zinazokabili nchi yetu
- Uongozi na Usimamizi: Tunahitaji Uongozi imara ili kuweza kusimamia rasilimali zetu kwa matumizi bora ya rasilimali.
- Miundombinu: Kiwango cha miundombinu, kama barabara na umeme, kinahitaji kuboreshwa ili kuimarisha uchumi.
- Elimu na Ujuzi: Kuimarisha elimu na mafunzo ni muhimu ili kutoa nguvu kazi iliyo na ujuzi wa kutosha.
Kwa kutumia vizuri rasilimali zilizopo, Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuwa nchi tajiri. Hata hivyo, inahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa serikali, sekta binafsi, na jamii ili kufikia malengo hayo.
#SisiNiTanzania #NaipendaNchiYangu #HayaNdioMatokeoChanyA #SSH #Kaziiendelee
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania ni tajiri kutokana na Rasilimali zilizopo, hivyo simamizi na matumizi thabiti ya hizo Rasilimali ni muhimu, pia ni wajibu wa Kila Mtanzania kuhakikisha tunatumia vyema Rasilimali zilizopo.
ReplyDeleteNi kweli kama alivyosema Rais tuna rasilimali za kutosha kwa mfano kwenye sekta ya madini kukiwa na teknolojia thankti madini yetu yataongezeka thamani uchumi utakua
ReplyDelete#sisinitanzania
#kaziiendelee
#SSH
Ni kweli Tanzania sio maskini kwa kuwa tumebarikiwa rasilimali nyingi sana kama madini, ardhi,wanyama, milima na misitu ambayo ikitumika vizuri itakuza uchumi wa Taifa letu na la mtu mmoja mmoja #sisinitanzania#siondototena#matokeochanya#kaziiendelee
ReplyDeleteTanzania ni mojawapo ya nchi zenye madini mengi barani Afrika kama vile dhahabu, Shaba, almasi, makaa ya mawe, chuma, gesi asilia na Tanzanite (jiwe la thamani linalopatikana Mererani-Tanzania pekee.
ReplyDeleteKwenye sekta ya utalii; Tanzania ni moja ya nchi maarufu duniani kwa utalii wa mazingira na wanyamapori. Ina mbuga za wanyama, fukwe za bahari ya Hindi na mlima Kilimanjaro, mlima mrefu barani Afrika.
Utamaduni na Lugha.
Tanzania ina makabila zaidi ya 120, kila moja likiwa na tamaduni, lugha, na urithi wake wa kipekee. Lugha ya Kiswahili pia ni moja ya urithi mkubwa wa kitaifa na nyenzo muhimu ya kuunganisha watu. Kiswahioli ni lugha inayozungumzwa Afrika mashariki na inawndelea kusambaa kwenye nchi zinhine nyingi duniani.
Miundombinu na Fursa za Biashara.
Miradi mikubwa ya miundombinu, kama reli ya kisasa ya SGR, bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP), na bandari za kimkakati, inazidi kuimarisha uwezo wa uchumi wa Tanzania.
Ni kweli Tanzania siyo nchi masikini tuna rasilimali nyingi sana , hatuna tu ufanisi wakutosha. Katika kuzitumia rasilimali zetu
ReplyDeleteNakubaliana na hoja hii kwasababu Tanzania tumebarikiwa na rasilimali mbali mbali katika kila sekta kama vile Madini, Kilimo,Utalii,Nishati .
Delete, Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuwa nchi tajiri. Hata hivyo, inahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa serikali, sekta binafsi, na jamii kwa ujumla.
#SisiNiTanzania #NaipendaNchiYangu #HayaNdioMatokeoChanyA #SSH #Kaziiendelee