Jumatatu, 18 Novemba 2024

Jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (Maternity Wing) 


Ni moja ya miradi ya afya ya kisasa iliyojengwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na maeneo jirani. Jengo hili linafanikiwa kutoa huduma za uzazi kwa viwango vya juu, likiwa limejengwa na vifaa vya kisasa kama vile:

  1. Vyumba vya upasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito.
  2. Vyumba vya kujifungulia vilivyoboreshwa.
  3. Vitengo vya kuhudumia watoto njiti na walioko kwenye hali mahututi (NICU).
  4. Sehemu za wagonjwa wa nje (OPD) za huduma ya mama na mtoto.
  5. Nyumba za kulaza wagonjwa (wards) zenye mazingira rafiki kwa mama na mtoto.


Jengo hili ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya afya, kupunguza vifo vya uzazi, na kutoa huduma bora kwa jamii. Limechangia kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa dharura, hususan kwa akinamama wa vijijini na maeneo ya mbali.



Maoni 17 :

  1. Afya Ndio Msingi wa binadamu kuelekea nyanja zote za kiuchumi, bila afya hakuna kitu kitaendelea.
    Dr Samia ameboresha Sekta ya afya kila Kona ya Tanzania kuhakikisha Wananchi wanapata huduma Bora

    JibuFuta
  2. Kazi nzuri,jitihada za mhe Rais katika sekta ya Afya zinaonekana, tunaona wilaya nyingi sana kuna uwepo wa vituo vya Afya,Hosptali za Wilaya na Zahati mbalimbali..Mhe Rais kagusa Mkoa,Wilaya hadi katika kata #Sisinitanzania #SSH #Tanzania

    JibuFuta
  3. Ili nchi ikue kiuchumi inahitaji wananchi wenye Afya bora na hili Raisi wetu ya awamu ya sita amelionesha kwa ujengaji, ukarabati na ununuzi wa vifaa tiba katika maeneo mengi nchini

    JibuFuta
  4. Hongera nyingi kwa serikali yetu ya awamu ya 6 huduma za afya zimesogezwa karibu na kila mwananchi ambapo inasaidia katika uimara wa afya na kuongezeka kwa uzalishaji. Kwani afya bora ndio msingi wa uchumi wetu.

    JibuFuta
  5. Sekta ya afya ni moja ya sekta zenye umuhimu mkubwa nchini katika kulifanya taifa la watu wenye afya bora ili kuongeza nguvu kazi ya uzalishaji mali na kushiriki katika harakati nyengine za kiuchumi. Aidha, kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Katika kufikia hayo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan ameimarisha sekta ya afya kwa kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya aidha kwa kujenga up ya au ukarabati wa miundombinu ya afya kote nchini, ununuzi wa vifaa tiba na kuongeza upatikanaji wa uhakika wa Madawa na huduma za kibingwa za kitabibu. Vituo vya mama wajawazito na clinic za watoto zimejengwa na kuwekewa mazingira rafiki ya utoaji huduma za kibingwa na kitaalamu kuhakikisha tunapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto. #Sisinitanzaniampya #Nchiyetukwanza #Nahayanimabadilikochanya #DrSSH #Awamuyasita #Kaziiendelee

    JibuFuta
  6. Kazi ya mama samia, rais aliyeamua kufanya kazi kwa kuwatumikia wananchi. Matokeo ndio haya sasa tunayaona, hakika unazidi kutupa iman kubwa sana watanzania

    JibuFuta
  7. Kwa kweli raisi wetu mpedwa #SSH ameimarisha huduma za afya pongezi zake apewe amemgusa kila mtanzania
    #matokeochanya

    JibuFuta
  8. Tuache utani bila kutaja eneo ningejua ulaya!haya sasa wamama kazi kwenu serikali ishafanya sehemu yake...lete nguvu kazi ya taifaaa!!

    JibuFuta
  9. Ila wahudumu,madaktari wapo?yasije yakawa majengo tu huduma hazieleweki

    JibuFuta
  10. Afya ni jambo muhimu na la msingi kwa binaadam, ili kuhakikisha taifa lipo imara hatuna budi kuona rai wake wakiwa na afya njema kwa mantiki hii serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa dr Samia Suluhu Hassan wamefanya kazi kubwa katika kuimarisha sekta ya afya nchini na haya ndio matokeo yake kwa upande wa afya ya mama na mtoto:-
    MATOKEO: Kutokana na. uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hasssan katika kuimarisha ubora wa huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ambapo kupitia Viashiria vikuu vinavyotumika kupima mwenendo wa ubora wa huduma kwa Nchi Wanachama wa Shirika la Afya Duniani imejidhihirisha wazi kuwa Nchi yetu imefanya vizuri sana katika kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto katika kipindi cha awamu ya 6 hii ni pamoja na:-
    _Ongezeko la Wajawazito waliojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
    idadi ya wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya Nchini imeendelea kuongezeka kutoka asilimia 63 mwaka 2021 hadi asilimia 85 mwaka 2023. Lengo la nchi ni kufikia asilimia 95 ya wanaojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ifikapo mwaka 2030.
    _Tumepunguza vifo vya wanawake wajawazito kwa asilimia 80 Kuimarika kwa huduma za uzazi, mama na mtoto kumepelekea kupunguza vifo vya wajawazito vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa sasa.
    _ vifo vya watoto umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2022.
    _ vifo vya watoto umri chini ya mwaka mmoja vimepungua kutoka vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 33 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi sasa,
    _vifo vya watoto wachanga (wenye umri wa chini ya siku 28) vimepungua kutoka 25 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi vifo 24 kwa vizazi hai 1,000 hadi sasa
    #SisiNiTanzania #HayaNdioMatokeoChanyA #drsamia

    JibuFuta
  11. Huduma za Afya ya mama na mtoto zimesaidia kupunguza vifo, kukuza uelewa wa umuhimu wa wanawake kujifungulia hospitalini hasa kwa wanaoishi vijijini, kuo gezeka kwa wataalamu wa afya na vifaa tiba na pia kukuza uchumi kwani vifo vya kina mama vinaweza kuathiri ukuaji wa jamii, uchumi na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
    Hivyo basi tunamshumuru na kumpongeza Raisi wetu kwa juhudi zake katika sekta ya Afya.
    #sisinitanzania
    #matokeochanya
    #SSH

    JibuFuta
  12. Huduma ya afya ya mama na mtoto inahakikisha afya ya mama kabla na baada ya kujifungua.
    Huduma za kabla ya kujifungua (antenatal care) na baada ya kujifungua (postnatal care) hutolewa katika kitengo maternity wing. Hii inahusisha uchunguzi wa kiafya, ushauri kuhusu lishe, na kusaidia mama kupata nafuu baada ya kujifungua. Kuhakikisha ustawi wa mama na mtoto

    JibuFuta
  13. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  14. Haya yote nimatokeo ya ongezeko la miundombinu za huduma za afya ambapo takribani 1061 za miundombinu zimejengwa katika miaka mitatu 3 ya uongozi wa rais dkt Samia Suluhu Hassan

    JibuFuta
  15. Mtaji wa kwanza kwa binadamu ni AFYA, bila afya taifa haliwezi kuendelea kwa namna yoyote ile kwa maana hakutakuwa na nguvu kazi ya kuendesha Taifa kiuchumi, kijamii, kisiasa wala kiutamaduni. Hivyo, Raisi anayetoa kipaumbele kwa afya za wananchi wake ana maono makubwa sana kwa taifa analoliongoza.
    #ssh
    #matokeochanya
    #sisinitanzania
    #kaziiendelee
    #nchiyangukwanza

    JibuFuta
    Majibu
    1. Serikali ya Rais wetu daktari Samia Suluhu Hassan inafanya kazi kwa vitendo hakuna porojo mama akisema hakuna vifo vya mama na mtoto anafanya kwa vitendo tunajivunia sana watanzania wote umetuokoa #sisinitanzania #nchiyangukwanza

      Futa
    2. Kazi ya mama yetu Dr.Samia Suluhu Hassan ameweza kufungua huduma ya mama na mtoto katika sekta ya afya. Ni mama mwenye utu ameweza kujali afya za wananchi wake
      Mama anaweza ,ana busara
      #ssh
      #matokeochanya
      #sisinitanzania
      #kaziiendelee
      #nchiyangukwanza

      Futa

VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA

Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...