Jumapili, 17 Novemba 2024

G20 SUMMIT: INDIA
India kama mwanachama wa G20 inanufaika vipi na Tanzania kwa njia mbalimbali, hasa kupitia biashara ya bidhaa, uwekezaji wa moja kwa moja, na ushirikiano wa maendeleo. Mchango wa Tanzania kwa uchumi wa India ukoje na je unauwiano?

Tanzania na India zimeonesha dhamira ya kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora za kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande zote mbili kama ifuatavyo;

1.⁠ ⁠India ni mshirika wa tatu kwa ukubwa wa kibiashara na Tanzania na imekuwa miongoni mwa wawekezaji watano bora kwa kuwekeza Dola za Kimarekani bilioni 4.58 kwa mwaka 2021/22. Usawa wa kibiashara katika mwaka huo ulikuwa sawa na miradi 630 ya uwekezaji yenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 3.68 iliyozalisha ajira mpya 60,000

2.⁠ ⁠Sekta nyingine wawekezaji wa India walizowekeza nchini Tanzania ni pamoja na afya, elimu, maji, teknolojia ya Habari na mawasiliano. Mfano, Mwezi Juni 2022 tulishuhudia kampuni sita kutoka India zikisaini kandarasi ya uchimbaji wa visima vya maji katika miji 28 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 500, kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha watanzania milioni sita (6) kupata maji safi na salama.

3.⁠ ⁠Aidha, uhusiano huu umekuwa chachu ya upatikanaji wa soko la mbaazi za Tanzania tani 200000 nchini India  na kushawishi wawekezaji kitoka nchini india kuja kuwekeza katika viwanda vya  kuongeza thamani katika mazao ya kilimo ambayo husafirishwa zaidi katika nchi hiyo ikiwemo Mbaazi na Parachichi ili kuongeza ajira na pato la Taifa  pamoja na kuhakikisha soko la mazao hayo linalotabirika.
MJADALA

[17/11/2024, 14:18:45] ~ @shuukorosho: India ni mununuzi mkubwa wa bidhaa ya parachichi kutoka Tanzania. Kwa mara kwanza 2022 Tanzania imefanikiwa kupeleka kiasi kikubwa cha zao la Parachichi nchini India. Ambapo Kontena la Parachichi futi 40 ambalo ndani yake kuna'trays' za parachichi 5700. Maparachichi hayo yaliingizwa nchini India kupitia Kampuni ya IG Fruits ya nchini India kwa kushirikiana na wakulima pamoja na Kampuni ya Avoafrica yenye ofisi zake Makambako Mkoani Iringa ambayo itasaidia kufungua fursa nyingi za masoko kwa wakulima wa zao hilo nchini Tanzania ikiwemo ajira na kusababisha kuongezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja.

[17/11/2024, 14:37:09] ~ Novatus CP💊💉: Pamoja na nchi ya India kuwa mnunuaji wa Korosho Tanzania na kusaidia kukua kwa uchumi wa Tanzania na India, Tanzania inafaidika kibiashara nchini india kwa kuwa muuzaji wa dhahabu, mazao ya mboga zilizokaushwa

Mwaka 2023 Tanzania ilifanikiwa kupata soko la dawa malighafi nchini india (Penicillins and its derivatives) zenye thamani ya dola za kimarekani millioni 28.19. Mathalani, India imekuwa na msaada mkubwa sana katika sekta ya afya Tanzania hususani katika huduma za dawa ambapo mwaka 2023, dawa zenye thamani ya  takribani 193M USD ziliingizwa nchni kutoka India.

[17/11/2024, 14:43:30] ~ lubelamd457: Tanzania inapata mapato mengi kwa kuuza korosho India, pia tunapata fedha za kigeni ambazo ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na inachangia katika upatikanaji wa ajira kwa wakulima na wafanyakazi katika sekta ya kilimo.

Ingawa nchi yetu inapata faida kutokana na mauzo ya korosho, masuala ya usawa katika biashara yanaweza kuonekana zaidi, hasa pale ambapo tutaongeza thamani kwenye korosho zetu kabla ya kwenda kuziuza India , kwasababu India wanapata manufaa makubwa zaidi kwa kuongeza thamani na kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani.

[17/11/2024, 14:53:11] ~ Mr Mngazija: Tanzania ina nafasi kubwa ya kutumia mwanya huo ili kuongeza mauzo yake nchini India hasa mazao ya kilimo Korosho, Pamba,kahawa, Chai, Viungo na Ngozi za Wanyama. India ni mlimaji na mtumiaji mkubwa wa nafaka aina ya pulses [mbaazi, kunde choroko] ambazo zinapatikana kwa wingi T

[17/11/2024, 15:29:43] ~ salumsay396: India inanufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na uhusiano mzuri wa kibiashara uliopo Kati yake na Tanzania, kiufupi malighafi nyingi kwa ajili ya kulisha viwanda vyake huwa zinatoka Tanzania. Tanzania ni soko la mazao mengi ambayo yamekuwa na uhitaji mkubwa kwa Nchi ya India kama vile mbaazi, korosho, kahawa n.k



[17/11/2024, 15:44:26] ~ Peter: India kama mwanachama wa G20 ina nafasi kubwa ya kunufaika kutoka Tanzania katika maeneo mbalimbali, hasa kupitia biashara ya bidhaa, uwekezaji wa moja kwa moja, na ushirikiano wa maendeleo. Hapa kuna baadhi ya njia ambazo India inaweza kunufaika na Tanzania:

### 1. Biashara ya Bidhaa
•⁠  ⁠*Uuzaji na Ununuzi:* Tanzania ina bidhaa mbalimbali kama kahawa, chai, na bidhaa za kilimo ambazo India inaweza kuagiza. Kwa upande mwingine, India inaweza kupeleka bidhaa zake za viwandani, dawa, na bidhaa za teknolojia kwa soko la Tanzania.
•⁠  ⁠*Fursa za Masoko:* Taarifa za soko na fursa za biashara zinaweza kuongezeka, na hivyo kusaidia makampuni ya India kufikia masoko mapya na kuimarisha uwepo wao barani Afrika.

### 2. Uwekezaji wa Moja kwa Moja
•⁠  ⁠*Uwekezaji katika Sekta za Kistratejia:* India inaweza kuwekeza katika sekta kama vile nishati, miundombinu, na kilimo nchini Tanzania. Uwekezaji huu unaweza kuleta teknolojia mpya, ufundi, na ajira kwa watu wa Tanzania.
•⁠  ⁠*Kukuza Uhamasishaji wa Biashara:* Kwa kuanzisha viwanda na kampuni nchini Tanzania, India inaweza kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania huku ikijenga faida za kiuchumi kwa uwekezaji huo.

### 3. Ushirikiano wa Maendeleo
•⁠  ⁠*Miradi ya Maendeleo:* India inaweza kushirikiana na Tanzania kwenye miradi ya maendeleo kama vile elimu, afya, na teknolojia, ambayo inaweza kuleta manufaa kwa jamii za Tanzania na kuongeza ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
•⁠  ⁠*Mpango wa Utekelezaji wa Sera:* Ushirikiano katika utafiti wa wakulima na uboreshaji wa mazoea ya kilimo unaweza kuongeza uzalishaji wa chakula na kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

### Mchango wa Tanzania kwa Uchumi wa India
•⁠  ⁠*Malighafi na Rasilimali:* Tanzania inatoa malighafi kama vile madini, bidhaa za mazao, na malighafi nyingine kwa ajili ya viwanda vya India, hivyo kuchangia katika uzalishaji wa bidhaa.
•⁠  ⁠*Masoko ya Bidhaa:* Tanzania inatoa soko muhimu la bidhaa za India, hasa katika sekta za dawa na bidhaa za matumizi ya kila siku.

### Uwiano wa Kibiashara
Uwiano wa kibiashara kati ya India na Tanzania umeimarika katika miaka ya hivi karibuni, ingawa bado kuna nafasi kubwa ya kukuza uwiano huu zaidi. Mifano ya ushirikiano ni pamoja na makubaliano ya biashara na jumuiya za kiuchumi ambazo zinaweza kuimarisha uhusiano wa kibiashara.

Kwa ujumla, India na Tanzania wanaweza kunufaika kwa pamoja kupitia ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji wa moja kwa moja, na miradi ya maendeleo, ambayo itaimarisha uchumi wa nchi hizo mbili na kuchangia katika ukuaji wa jumla wa kikanda na kimataifa.



[17/11/2024, 15:48:26] ~ Jeremy96: India na Tanzania kwa pamoja wanaweza faidika kupitia ushirikiano wa biashara, Uwekezaji, na uwekezaji,,sababu kubwa ni uhitaji wa baadhi ya mazao toka Tanzania kama vile Korosho..hii inaweza kuleta athari chanya kwa Tanzania kwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
[17/11/2024, 15:51:54] ~ Kidebeli: https://www.instagram.com/p/DCeRkPbosZ4/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==

[17/11/2024, 15:52:03] ~ Mjamaa_halisi: India Ni Nchi Ya Nne kwa kufanya Biashara Kwa Wingi Tanzania, biashara Hiyo Inakadiriwa kuwa na Dola Za Kimarekani Billion 6.5 kwa Mwaka 2022/2023. Kwa Kushirikiana na Vyama Vya TANECU&MAMCU!!.
Hata hivyo Poah ni Miongoni mwa Vyanzo vikuu Vitano Bora Vya Uwekezaji Vinavyoingia Tanzania. Kwa mwaka Wa Fedha 2021/2022 miradi 360 yenye dollar Billion 3.7 ilisajiliwa na TIC.
 Ushirikiano baina Ya Tanzania Na India ni chachu Ya Kufungua uwekezaji Nchini  ikiwa serikali imeendeleza Jitihada za Kuimarisha Uhusiano wa Karibu Na Nchi Ya Indiakwani Korosho Zinazizalishwa Tanzania Husafirishwa Hadi India Kwa ajili Ya Kubanguliwa ..
Furthermore, viwanda Vyetu 6 vya Kubangulia Korosho vyenye Uwezo wa Tani 28,600/:  hushirikiana na India Kuhakikisha Kwa Mwaka Zaidi ya Tani za Korosho 64,000/: zinabanguliwa!! Hivyo Ushirikiano wetu ni Chachu Ya Fursa Tanzania Kupata Uwekezaji mkubwa Wa Viwanda, Biashara Na Hata Kilimo lengo ni Kukuza Uchumi na Kupelekea Ajira Nyingi Zaidi kwa Watanzania.. 
🇹🇿🙏🏻

[17/11/2024, 15:53:53] ~ 45: Kama India inavyotegemea Tanzania  kama source ya chakula Chao muhimu wao wananufaika kwa hilo.
Lakini Tanzania inanufaika kuimarisha uchumi hasa sekta ya biashara ya korosho, pia kumarisha sekta ya kilimo cha korosho na kufungua milango ya ajira kwa vijana kama wataamua kuiona fursa ya kilimo cha korosho na kukuza vipato vyao.
Taifa litapata makusanyo ya kodi na kuendeleza miradi mbalimbali.

[17/11/2024, 15:56:51] ~ Aalliya🥰: Uhusiano huu unasaidia kuboresha maisha ya watu wa Tanzania kwa kuleta teknolojia mpya na maarifa kutoka India, ambayo yanaweza kusaidia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
[17/11/2024, 15:57:24] ~ Aalliya🥰: Katika sekta ya teknolojia, Tanzania imefaidika sana kutokana na uhusiano wake na India. Hapa kuna mifano kadhaa:

1.⁠ ⁠Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT): India ni kiongozi katika sekta ya ICT, na kampuni nyingi za India zimewekeza nchini Tanzania. Kwa mfano, kampuni kama TCS (Tata Consultancy Services) zinatoa huduma za IT na ushauri, ambazo zinasaidia kuboresha mifumo ya teknolojia nchini.

2.⁠ ⁠Kilimo: India inatoa teknolojia za kisasa za kilimo, kama vile mbegu bora na vifaa vya umwagiliaji. Hii inasaidia wakulima wa Tanzania kuongeza uzalishaji na kuboresha ubora wa mazao yao.

3.⁠ ⁠Nishati: India ina uzoefu mkubwa katika uzalishaji wa nishati mbadala, kama vile nishati ya jua. Tanzania imeweza kujifunza kutoka kwa India na kuanzisha miradi ya nishati ya jua ambayo inasaidia katika kuongeza upatikanaji wa umeme vijijini.

4.⁠ ⁠Afya: India ni maarufu kwa uzalishaji wa dawa na vifaa vya matibabu. Uhusiano huu umesaidia Tanzania kupata dawa za bei nafuu na vifaa vya matibabu, hasa katika kukabiliana na magonjwa kama malaria na VVU.

Hivyo, kwa ujumla, teknolojia kutoka India inachangia sana katika maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali.

[17/11/2024, 16:00:01] ~ Kidebeli: India na Tanzania ni washirika wazuri kibiashara 
Mauzo ya Tanzania kwa India- Tanzania inauizia India mazao ya kilimo kama korosho, pamba, kahawa, chai, ngozi za wanyama nk: bidhaa za misitu zikiwemo mbao na bidhaa za madini na vito vya thamani zikiwemo dhahabu, almasi nk.

Mauzo ya India kwa Tanzania - India inauizia Tanzania bidhaa  mbali mbali zikiwemo mashine, bidhaa za nguo, zana za kilimo, zana za usafirishaji, madawa, vifaa vya ujenzi, nafaka, bidhaa za matumizi, mitaji nk.

Tanzania ina nafasi kubwa ya kutumia mwanya huo ili kuongeza mauzo yake nchini India hasa mazao ya kilimo. India ni mlimaji na mtumiaji mkubwa wa nafaka aina ya pulses [mbaazi, kunde choroko nk.] ambazo zinapatikana kwa wingi Tanzania.

[17/11/2024, 16:02:47] ~ basilididaudi52@gmail.com: Ushirika wa India na Tanzania katika shuguli za kibiashara hasa zao la korosho itasidia 
1.kongeza uzalishaji wa zao hilo katika maeneo yanayolima korosho na kupelekea kuinua hali ya maisha ya wananchi na Ushirikiano huo watanzania na India 
Pia itasaidia kufungua milango kwa sekta zingine za kiuchumi na kijamii kama vile elimu na afya


[17/11/2024, 17:03:31] ~ Lizzah: India ni Nchi muhimu sana kwa Tanzania kwani ni nchi ya tano kwa uwekezaji na biashara nchini Tanzania ambapo wawekezaji  kutoka India wamewekeza mtaji wa kiasi cha dola za Marekani billion 3.7. Kama tujuavyo kabla ya Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hassan kwenda nchini humo kwa ziara ya kikazi Tanzania ilikua ikitozwa ushuru wa asilimia 35 kwa kuingiza Korosho zilizo banguliwa nchini humo lakini kupitia shujaa wetu Rais wetu Samia Suluhu Hassan rasmi Nchi hiyo imeondoa ushuru huo na Korosho zinaingia India bila Kodi 
 #Samiasuluhu #kaziiendelee🇹🇿

[17/11/2024, 17:27:05] ~ Kemibaro: Tanzania inauzia India mazao ya kilimo kama korosho, pamba, kahawa, chai, viungo, ngozi za wanyama nk: bidhaa za misitu zikiwemo mbao na bidhaa za madini na vito vya thamani zikiwemo dhahabu, almasi nk.

Mauzo ya India kwa Tanzania - India inauizia Tanzania bidhaa  mbali mbali zikiwemo mashine, bidhaa za nguo, zana za kilimo, zana za usafirishaji, madawa, vifaa vya ujenzi, nafaka, hivyo kwa mtiririko huo unaona bado India anategemea sana uwepo wa Tanzania,kwa kuhitaji marighafi zinazopatikana hapa nchini,japo 
Tanzania ina nafasi kubwa ya kutumia mwanya huo ili kuongeza mauzo yake nchini India hasa mazao ya kilimo. India ni mlimaji na mtumiaji mkubwa wa nafaka aina ya pulses [mbaazi, kunde choroko nk.] ambazo zinapatikana kwa wingi Tanzania. mwaka 2011 iliagiza Tani 350,000 za pulses kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na kwamba mwaka huu 2012 uagizaji wa pulses unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 20 zaidi.hivyo watanzania tuzidi kujikita kwenyenye  kilimo.






Maoni 3 :

  1. India inauhusiano wa moja kwa moja na Tanzania kupitia biashara ya mazao kama korosho na mbaazi hivyo kuongeza pato la taifa na wakulima kwa ujumla

    JibuFuta
  2. Tanzania kama nchi yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo inaweza kufaidika na mipango ya G20 kuhusu usalama wa chakula, hususan kupitia ufadhili wa teknolojia za kilimo na masoko ya kimataifa kwa mazao ya kilimo kama kahawa, chai, korosho, na mbogamboga.

    JibuFuta
  3. Kwa kweli nchi inazidi kuchanja mbuga kwa kikubwa kwani inashirikiana vizuri na India katika sekta mbalimbali na pia imekuwa mnunuzi mzuri wa korosho zetu na hivyo kuongeza Pato la Taifa #sisinitanzania#siondototena#matokeochanya#kaziiendelee#ssh

    JibuFuta

VIJANA WAVUNA DHAHABU YA SAMAKI ZIWA VICTORIA: UWEKEZAJI WA VIZIMBA NA UMEME WA JUA CHINI YA UFADHIRI WA TADB WAFUNGUA MILANGO YA AJIRA NA UTAJIRI MPYA TANZANIA

Ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba ndani ya Ziwa Victoria umeanza kuwa nguzo muhimu ya kuimarisha uchumi wa vijana na kuchangia usalama w...