Jumanne, 28 Oktoba 2025

RIPOTI YA HALI YA UCHAGUZI MKUU – TANZANIA

Tarehe: 29 Oktoba 2025

Muda: Asubuhi (kuanzia saa 12:30 alfajiri – 02:10 asubuhi)
Chanzo: Taarifa za moja kwa moja kutoka kwa wananchi walioko vituoni maeneo mbalimbali nchini.

Muhtasari wa Jumla wa Hali ya Uchaguzi

Asubuhi ya leo Watanzania wamejitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura nchi nzima. Hali ya jumla imeendelea kuwa shwari, yenye amani, usalama na utulivu.
Vituo vingi vimefunguliwa kwa wakati, maandalizi yamekamilika na wapiga kura wanafuata taratibu kwa utulivu.

Mwitikio mkubwa umeonekana takribani mikoa yote iliyoripotiwa, na raia wengi wakisisitiza umuhimu wa kutimiza haki ya msingi ya kikatiba kupiga kura.

Ripoti kwa Mujibu wa Mikoa na Maeneo

✅ Dodoma

  • Bahi – Mwitikio mzuri wa wananchi; hali ni shwari.

  • Kongwa – Uhamasishaji mkubwa, wananchi wanaendelea kupiga kura kwa amani.

Mazingira: Rafiki, ulinzi umeimarishwa, utaratibu unazingatiwa.


✅ Simiyu

  • Bariadi Mji – Kituo cha Majengo

    • Kimefunguliwa mapema

    • Majina yamebandikwa vizuri

    • Makarani wanatoa maelekezo

    • Zoezi lilianza saa moja kamili asubuhi



✅ Kilimanjaro

  • Same – Wapiga kura wamejitokeza mapema, usalama na hamasa kubwa kuripotiwa.



✅ Kagera

  • Karagwe – Mvua ndogo inakumba eneo lakini bado wananchi wanaendelea na zoezi bila kusita.



✅ Lindi

  • Lindi Manispaa

    • Shughuli za kupiga kura zinaendelea sambamba na shughuli za uchumi

    • Biashara zimefunguliwa na usafiri unaendelea kama kawaida

  • Ruangwa – Malolo

    • Zozi linaendelea vizuri tangu mapema

  • Mtama – Nang’aka

    • Wapiga kura wanatiki na kurejea nyumbani kwa utulivu


✅ Rukwa

  • Nkasi – Nkomolo
    Zoezi linaendelea kwa amani.

  • Sumbawanga – Mtaa wa Chemka 1
    Foleni inaendelea, uhamasishaji ni mzuri.

    Wananchi wakiendelea kupiga kura katika kituo cha MTAA WA CHEMKA-1 kilichopo mtaa wa Chemka Kata ya Msua Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.

    Utulivu wa kutosha kijiji cha Isunta, kata ya isunta halmashauri ya wilaya ya nkasi, mkoa wa Rukwa.


✅ Njombe

  • Makambako – Kivavi
    Hali ya utulivu, wananchi wapo vituoni mapema.


✅ Mtwara

  • Masasi Mjini – Migongo, Nangaya A
    Zoezi linaenda kwa utaratibu mzuri; wananchi wanatimiza haki kisha kurejea kwenye shughuli zao.




✅ Mwanza

  • Nyamagana – Nyamanoro, Kituo cha Nkubi
    Mwitikio upo lakini changamoto ndogo:

    • Baadhi ya makarani hawatoi msaada wa kutosha kwa wapiga kura.
      (Taarifa imetolewa kwa mujibu wa mwakilishi)


✅ Kusini Unguja na maeneo mengine

— Hakuna changamoto kubwa zilizoripotiwa katika taarifa za asubuhi.


✅ AUSHA

Mtaa wa Korongoni, Kata ya Lemara, Wilaya ya Arusha Mjini wananchi wanaendelea na zoezi la kupiga kura ili hali vifaa vilichelewa kidogo. Kuna utulivu.


Wilaya ya Namtumbo,Kata ya Namtumbo,Mtaa wa Lusenti,Kituo cha Lusenti.



3️⃣ Uhamasishaji na Ushiriki wa Wananchi

Ujumbe mwingi wa hamasa umetolewa na wananchi, ukiwahimiza wengine kujitokeza mapema na kutimiza wajibu wao wa kikatiba:

“Siku niliyoisubiri na kuiombea kwa ham ni leo… Nimetimiza haki yangu ya msingi ya kikatiba kupiga kura.”

Hashtags zilizotumika sana:
#KidoleNaWino ✅ | #KidoleNaTiki ✅ | #NdioLeo


4️⃣ Usalama na Taratibu

  • Ulinzi umeimarishwa katika vituo vingi

  • Makarani wanaongoza utaratibu vizuri

  • Hakuna vurugu wala taharuki kuripotiwa asubuhi hii


5️⃣ Changamoto Zilizobainishwa

  • Huduma kwa wapiga kura: Mwanza (Nyamanoro) – usaidizi kwa baadhi ya wapiga kura si wa kuridhisha

  • Hali ya hewa: Karagwe – mvua ndogo lakini hakuna athari kubwa


6️⃣ Hitimisho la Awali

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 umeanza kwa muitikio mkubwa, amani na utulivu. Wananchi wanaendelea kutimiza wajibu wao kwa nidhamu na uzalendo.

Ripoti hii itaendelea kusasishwa kadri taarifa mpya zinavyopokelewa kutoka vituo mbalimbali nchini.



TATHMINI YA KINA YA MJADALA WA TANZANIA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

 

Baraza la Wazee wa TANU Sheikh Suleiman Takadir wa pili chini kulia, wa pili waliosimama Dossa Aziz, wa sita Julius Nyerere, wa saba John Rupia, wa tisa Said Chamwenyewe, anayefuatia Jumbe TambazaMshume Kiyate.

UTANGULIZI: Misingi ya Mjadala

Mjadala huu wa TikTok uliofanyika kwa siku tatu mfululizo, umeonyesha mwamko wa Watanzania kuelekea uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ukijikita katika hoja ya msingi:

“Historia ya Tanzania inatufundisha nini kuelekea uchaguzi mkuu?”

Washiriki walijadili siasa, historia, amani, elimu ya uraia, na wajibu wa raia kwa umakini mkubwa.
Tofauti na mijadala mingi ya mtandaoni, huu ulitawaliwa na utulivu, umoja, hoja za kistaarabu, na uelewa wa kitaifa.

KIPINDI CHA KWANZA – KUJIKUMBUSHA HISTORIA YA UHURU

Uelewa wa historia uliojitokeza

Washiriki walikumbuka namna Tanzania ilivyopata uhuru wake:

  • Tanganyika (1961) kupitia TANU na Mwalimu Julius Nyerere;

  • Zanzibar (1963) kupitia ASP na Abeid Amani Karume;

  • Muungano (1964) uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli kama:

“Kujua tulikotoka ni kujuwa tunapokwenda”
ilionyesha kuwa washiriki wanaona historia kama dira ya taifa.

Kushoto: John RupiaJulius NyerereZuberi Mtemvu. Waliosimama nyuma yao ni BANTU Group Vijana Walinzi wa Viongozi wa TANU.

Uhusiano na uchaguzi wa sasa

Hoja kuu: uhuru ulipatikana kwa umoja, sio kwa ubaguzi — na uchaguzi wa leo unapaswa kuenzi misingi hiyo.
Mifano ilitolewa:

  • TANU na ASP ziliunganisha watu bila kujali dini, kabila, au rangi.

  • Hivyo, wapiga kura leo hawapaswi kugawanyika kwa misingi hiyo.

🟢 Uchambuzi wa kihistoria:
Hii inarudisha dhana ya Pan-Africanism — umoja wa Waafrika dhidi ya mgawanyiko wa kikoloni.
Mjadala ulionyesha kuwa Watanzania wengi bado wanaona umoja huu kama uti wa mgongo wa Taifa.



KIPINDI CHA PILI – MAANA YA UCHAGUZI NA AMANI

Kauli kuu zilizotawala

  • “Uchaguzi si uwanja wa vita bali ni maamuzi ya kupata viongozi sahihi.”

  • “Uchaguzi ni tukio la muda, amani ni urithi wa milele.”

  • “Tuilinde amani yetu, umoja na mshikamano.”

Washiriki walisisitiza kuwa Tanzania imekuwa mfano wa amani barani Afrika tangu enzi za Nyerere, hivyo amani hiyo si zawadi bali jukumu la kila raia.

Mfano wa kihistoria

Katika historia, Tanzania haijawahi kuwa na vita ya kisiasa wala mapinduzi ya damu tangu uhuru.
Hii ni tofauti na majirani kama:

  • Uganda (Idi Amin, 1971–1979),

  • Rwanda (Vita ya wenyewe kwa wenyewe 1994),

  • Kenya (vurugu za uchaguzi 2007).

Washiriki walitumia historia hiyo kuonya vijana:

“Tuna amani ambayo wengine wangeiua kuwa nayo; tusichezee moto huu wa umoja.”

KIPINDI CHA TATU – ELIMU YA URAIA NA VYOMBO VYA HABARI

🔹 Hoja kuu

  • “Bila elimu ya uraia ni rahisi mtu kuchukuliwa na propaganda badala ya hoja za kisera.”

  • “Watu wana post maudhui yaliyojaa uchochezi, tuwe makini.”

Washiriki waliona mitandao ya kijamii kama panga lenye makali mawili:
Inaweza kuelimisha au kuharibu.
Kauli ya kadogzwbij3 ilisisitiza:

“Tafuteni taarifa sahihi kwenye vyanzo sahihi.”

🔹 Uhusiano wa kihistoria

Waasisi wa taifa (kama Nyerere) walisisitiza elimu kama silaha ya ukombozi.
Mfano: Azimio la Arusha (1967) lilihimiza kujitegemea kwa maarifa.
Hivyo, elimu ya uraia leo ni mwendelezo wa falsafa hiyo — kuhakikisha demokrasia inategemea maarifa, si jazba.

KIPINDI CHA NNE – WAJIBU WA VIJANA

Ujumbe uliojitokeza

  • “Kura yako ni sauti yako.”

  • “Vijana tuache mihemuko, tufuatilie historia ya nchi yetu.”

  • “Jitokeze kupiga kura Oktoba 29.”

Washiriki vijana walionesha uelewa mkubwa wa majukumu yao.
Waliona kura kama “nguvu ya mabadiliko,” si silaha ya fujo.

Mfano wa kihistoria

Kizazi cha uhuru kiliongozwa na vijana:

  • Nyerere alikuwa na miaka 39 tu alipokuwa Waziri Mkuu (1961).

  • Karume alikuwa kiongozi wa vijana wa ASP kabla ya mapinduzi.

  • Hivyo, vijana wa leo wana wajibu wa kulinda walichoanzisha wazee wao — amani na uzalendo.

WADAU WALIOIBUKA KAMA SAUTI KUU

Jina la MshirikiDira KuuKauli ya Msingi
tukutu_kasukuUmoja na amani“Tuilinde amani yetu; sio nchi zote zinafurahia kutuona tuna amani.”
MyCountryTzElimu ya uraia, maadili ya wanasiasa“Bila elimu ya uraia, mtu anadanganywa na propaganda.”
TanzaniteUchaguzi wa amani“Uchaguzi si vita, bali ni maamuzi ya kupata viongozi sahihi.”
Uzuri wa mama tumeuonaHistoria na kizazi kipya“Kujua tulipotoka ni kujua tunapokwenda.”
Kadogzwbij3Habari sahihi na utulivu“Tafuteni taarifa sahihi kwenye vyanzo sahihi.”
Nyuki.22Uzalendo na ushiriki“Wino si tu rangi, ni sauti ya haki na wajibu.”
Davis DenisUkomavu wa kisiasa“Changamoto zipo hata kwenye familia; tusilishwe matango pori.”

MAJUMUIKO YA HOJA ZA KIJAMII NA KISIASA

MadaMaana kwa TaifaFundisho la Historia
AmaniNguzo ya maendeleoTanzania imedumu kwa amani tangu 1961.
Elimu ya uraiaKinga dhidi ya propagandaFalsafa ya Nyerere ya “kujua haki yako.”
Ushiriki wa vijanaMustakabali wa taifaVijana ndio waliokuwa nguzo ya uhuru.
KuraSauti ya wananchiTanganyika 1961 ilipata uhuru kwa kura za amani.
UmojaSilaha ya kudumuMuungano 1964 ni ushahidi wa mshikamano.


HITIMISHO: MWANGAZO WA TAIFA

Mjadala huu umetengeneza picha kamili ya raia anayekomaa kisiasa — anayejua:

  1. Kura si ushindani wa vyama, bali wajibu kwa taifa.

  2. Historia si simulizi ya kale, bali ni dira ya maamuzi ya leo.

  3. Amani na umoja ni tunu zisizoweza kubadilishwa na siasa za muda.

Kauli ya mwisho ya Davis Denis ilihitimisha kwa ufasaha:

“Amani tuliyorithishwa, tuitunze na tuipe kizazi kijacho. Changanya akili ya kuambiwa na zako.”

HITIMISHO KWA TAALUMA

Kihistoria, mjadala huu ni kioo cha utamaduni wa kisiasa wa Tanzania:

  • Umeonyesha urefu wa uvumilivu wa Watanzania tangu enzi za TANU hadi vyama vingi.

  • Umeonesha kuwa demokrasia yetu imekoma — watu wanazungumza kwa hoja, si jazba.

  • Ni dalili kuwa taifa limejenga utamaduni wa siasa zenye ustaarabu na busara.

Kama tulivyopata uhuru kwa umoja, basi tuilinde amani yetu kwa hekima.
Historia haipaswi kujirudia kama funzo lisilojifunzwa.

Jumapili, 26 Oktoba 2025

WATU, BABU NA BIBI ZETU MILIONI MOJA WALIKUFA AFRIKA MASHARIKI PEKEE WAKATI WA VITA VYA KWANZA VYA KIDUNIA,WAAFRIKA WENGI PIA WALIPIGANA HUKO ULAYA, WAKITETEA MASILAHI YA WAKOLONI WAO. LEO, THAMANI YAO IMESAHAULIWA KWA KIASI KIKUBWA.


Mnara wa ukumbusho wa kuvutia zaidi kwa wahasiriwa wa Kiafrika wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu (1914-1918) haupatikani barani Afrika bali uko Ufaransa.
Katika vita vya Delville, moja ya mapigano makali katika eneo la Somme mwaka wa 1916, Brigade ya 1 ya Infantry ya Afrika Kusini ilipata hasara kubwa na waafrika wengi waliuwawa.

Jeshi la Afrika Kusini ni mojawapo ya mashirika machache barani Afrika ambayo yanaheshimu na kuthamini mchango wa Askari Hawa waafrika. 

KUNA ufahamu mdogo kuhusu vita ya kwanza ya Dunia miongoni mwa watu weusi wa Afrika, hili limefanywa kusudi na wakoloni wa Afrika ili Historia hii isisimuliwe kabisa kwa uzao wa baadae wa Kizazi cha Afrika

WAKATI wa mzozo huo, takriban watu milioni 2 kutoka kote barani Afrika walihusika kikamilifu katika makabiliano ya kijeshi, kama wanajeshi au wabebaji mizigo, huko Ulaya na Afrika. Mwanzoni mwa vita, baadhi ya Waafrika walijitolea kushiriki, wakitiwa moyo na kudanganywa juu ya matarajio ya mapato ya kawaida. 



Kuanzia 1915, Wazungu walianza kuandikisha maelfu ya wanaume Waafrika. Wafaransa pekee walitumia wanajeshi wa Kiafrika 450,000 kutoka makoloni yao Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kupigana dhidi ya Ujerumani kwenye mstari wa mbele huko Ulaya.


Waafrika Milioni moja waliuawa Afrika Mashariki pekee


Vita vilipozuka Ulaya mwaka wa 1914, askari wa Kiingereza na Ufaransa walijitayarisha kuteka makoloni manne ya Wajerumani katika Afrika (Afrika Mashariki ya Kijerumani, Afrika Kusini-Magharibi ya Kijerumani, Togoland na Kamerun). 

Mapigano yalikuwa ya kikatili mno,haswa katika Afrika Mashariki ya Ujerumani ambapo Jenerali mkatili wa Ujerumani Lettow-Vorbeck alipitisha mkakati wa kuasi , kuteka na kuuwa katika maeneo mengi zaidi katika vita. Zaidi ya wabebaji 200,000 walisafirisha silaha, risasi na chakula kwa wanajeshi. Wakijulikana kwa jina "Askari mwaminifu" (neno la Kiswahili la 'askari') bado limebaki katika vitabu vya historia ya Ujerumani.

Kwa kweli kulikuwa na Uonezi wa ajabu
watu wengi walidakwa kutoka katika himaya zao na walidharauliwa na wakazi wa wenzao baada ya Kurudi nyumbani kutoka katika vita, walikosa mashamba. Mavuno yaliporwa na kuharibiwa na wanajeshi waliokuwa wakipita ili kuhakikisha kwamba hakungekuwa na chakula chochote kwa ajili ya wanaowafuatia. 

Hakuna takwimu sahihi zinazosema ni watu wangapi walikufa kwa njaa. Ukweli kwamba eneo la utawala wa kikoloni la Dodoma katika eneo ambalo sasa ni Tanzania lilipoteza asilimia 20 ya wakazi wake mwaka 1917/18 ni jambo hadi leo limeacha dalili fulani ya unyonge na sononeko kwa jamii ya kitanzania. 

Wanahistoria wanakadiria kuwa watu milioni moja walikufa Afrika Mashariki kutokana na vita hivyo. Mlipuko wa homa ya Kihispania, ambayo ilienea haraka, watu waliodhoofika muda mfupi baada ya vita kumalizika, ilisababisha vifo zaidi ya 50,000 hadi 80,000. 

"Vita vilibadilisha baadhi ya maeneo kwa kiasi kwamba yalihitaji miongo kadhaa kupona, hadi sasa athali zipo,alipata kusema Jürgen Zimmerer, profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha Hamburg.

Tanzania ya leo, iliyounda sehemu kubwa ya koloni la zamani la Afrika Mashariki ya Kijerumani, vita vya 1914-1918 kwa kiasi kikubwa havipo kwenye fahamu za Watanzania.Kizazi cha sasa kimesukumwa mbali na history hii"Ni kumbukumbu ambayo inazidi kutoweka, Wahusika wakuu wamekufa kwa muda mrefu. Walikuwa babu na bibi zetu!
kuanguka kwa himaya za kikoloni kunahusishwa na mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia." Ilikuwa ni kuenea kwa vuguvugu la uhuru wa mataifa ya Afrika kulikoanza mwanzoni mwa miaka ya 1950 ambako kuliwakilisha mabadiliko ya kweli na ambayo sasa yanaadhimishwa na sherehe za ukumbusho na sikukuu za kitaifa kukiwa bado na kovu baya lililojificha na Siasa,sheria na mitazamo ya Kikoloni.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia haiitaji sana Afrika kwa sababu historia kubwa lilikuwa ushindi kwa ujumla wa wakoloni huko ulaya ikiacha sehemu moja tu ya historia ndefu ya ushindi wa kikoloni na vitendo vya kikatili vilivyofanywa kwa watu wa Afrika wakati wa ukoloni. 



Katika muda wa miaka 75 ambayo Ubelgiji pekee ilitawala Kongo, watu milioni kumi walikufa. cha ajabu ni vita moja tu kati ya nyingi ndio zinatajwa sana," Zimmerer anasema. "Ukoloni ulikuwa wa kikatili kiasi kwamba idadi kubwa ya watu milioni moja haivutii hisia ambayo inapaswa - au ingetokea katika mazingira ya Ulaya.
Ulaya pia inachukulia mtazamo huu na kwa ujumla inapuuza mateso ya mamilioni ya Waafrika katika Vita vya Kwanza vya Dunia. Kwa maneno ya Zimmerer, vita barani Afrika "kwa ujumla huchukuliwa kama mzozo mdogo ambao hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa ama kuteseka.
Nijambo linalosikitisha sana.





Kagera River Girls: Uwekezaji wa Bilioni 4.1 Unaobadilisha Ndoto za Wasichana Kuwa Mafanikio ya Taifa

Katika Wilaya ya Karagwe, Kata ya Kanoni, kunasimama kwa fahari  Shule ya Sekondari Kagera River Girls —taa ya matumaini na ushahidi hai kwa...